Ujumbe kutoka Tanzania kwa Obama: Uwazi hujenga taasisi yenye nguvu
Rais wa Marekani Barack Obama na vyombo vya habari wanaweza kusafiri kuja katika nchi yangu wiki hii kwa majadiliano juu ya masuala ya 'mvuto' kama ya ushindani wa kiuchumi wa Marekani na China au amani na masuala ya usalama. Hata hivyo kama kweli Marekani ipo makini kuhusu kusukuma utawala wa kidemokrasia duniani kote, ni mambo haya madogo ya 'mvuto' ambayo ni muhimu zaidi.