Skip to main content
Policy Forum ina Bodi ya Wakurugenzi inayoakisi utofauti wa wanachama wake. Bodi ya Wakurugenzi hutokana na uchaguzi miongoni mwa wanachama. Bodi ya Wakurugenzi ya PF hukutana kila robo ya mwaka kwa ajili ya kupitia shughuli mbalimbali na kutoa mwongozo kwa sekretarieti. Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ni kama wafuatao:
Christina Kamili Ruhinda
Mwenyekiti wa Bodi
Contact Info
Education
Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Uongozi na Utawala, Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta, Kenya

Bi Christina Kamili Ruhinda ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Watoa Huduma za Kisheria Tanzania (TANLAP). Pia ni Mwenyekiti wa Songera - Songera - Mississippi Organization (SOMI), Tangible Initiative for Local Development (TIFLD), Tanzania Youth Inspiration Organization (TaYIO) na Door of Hope to Women and Youth Tanzania ( DHWYT)pia ni Mwanachama wa Kamati ya Usimamizi wa Kesi  iliyoanzishwa chini ya Waraka wa Jaji Mkuu Namba 5 ya 2018, ni Mwanachama mwanzilishi wa Mtandao wa Kikanda wa Afrika Mashariki wa Watendaji Walio na Wasio wa Serikali, ni Mwanachama wa Timu ya Msaada wa Kisheria ya Kitaifa ya Wizara ya Katiba na Sheria, mwanachama wa Mtandao wa Umoja wa wa Wanawake wa Kiafrika wa Kuzuia Migogoro na Usuluhishi (FemWise-Africa).

Bi Ruhinda ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika masuala ya Sheria, Haki za Binadamu, Jinsia, Uongozi, Uangalizi wa Uchaguzi, Mitandao, Usimamizi wa Programu na Ukuzaji wa Uwezo. Pamoja na mambo mengine, amekuwa akishiriki katika utambuzi wa maswala ambayo yameathiri upatikanaji wa haki nchini Tanzania.

Iku Lazaro
Mjumbe na Mweka Hazina wa Bodi
Contact Info
Education
Shahada ya Sayansi katika Ushuru, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Tanzania
Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Usimamizi wa Fedha na Uwekezaji, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Tanzania

Fatma ni Mkurugenzi wa Fedha aliye na uzoefu wa zaidi ya miaka 5 kwenye tasnia ya masuala ya fedha hasa kwenye sekta ya elimu kwa njia ya mtandao. Anaujuzi wa mipango katika biashara, mikakati, utafutaji fedha, bajeti, na usimamizi wa rasilimali fedha na watu. Fatma ana ujuzi wa uongozi, mawasiliano ya umma, usimamizi wa miradi na masuala ya kijamii

Fatma alizaliwa na kukulia nchini Tanzania; anapendelea kuona sekta ya elimu kama nyenzo ya kutokomeza umasikini barani Afrika na anaamini vijana wana nguvu na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya ulimwenguni. Tangu akiwa mtoto, Fatma amekuwa akishiriki katika kuwawezesha watoto, vijana na wanawake.

Semkae Kilonzo
Katibu wa Bodi
Contact Info
Education
Shahada ya Uzamili ya Uandishi na Vyombo Habari, Chuo Kikuu cha Cardiff, UK
Mafunzo ya Habari, Dublin, Ireland
Mafunzo ya Msingi ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji Jamii, Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini

Semkae Kilonzo alianza kazi Policy Forum mwaka 2007 kama mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uchechemuzi anayehusika na vyombo vya habari, ikiwa ni shauku ya mtandao kuona taarifa zinazohusiana na uchambuzi wa sera zikisambazwa kwa watunga sera, asasi za kiraia na umma kwa jumla. Akiwa kama mratibu na baadaye kama Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao amekuwa akiongoza Sekretarieti  katika majukumu ya kila siku ya kiofisi. Semkae pia ni mjumbe wa Kamati  ya Uwazi wa Bajeti, Uwajibikaji na Ushirikishwaji Global Movement for Budget Transparency, Accountability and Participation (BTAP).

Semkae ana digrii ya Uzamili ya Uandishi wa Habari kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff, Uingereza na pia amepata mafunzo kuhusu vyombo vya Habari, Dublin Ireland na pia katika  Shule ya Uandishi wa Habari Tanzania (TSJ). Semkae ni mhitumu wa mafunzo ya  Ufuatiliaji wa Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini. Semkae anapenda sana kuhamasisha ushiriki wa umma katika utengenezaji wa sera na matumizi ya rasilimali za umma yanayozingatia usawa.

Semkae hushiriki katika vikao vya Bodi ya Wakurugenzi kama Katibu wa Bodi.

Adv. Dominic Ndunguru
Mwenyekiti wa Bodi
Contact Info
Education
Shahada ya Uzamili ya Haki za Binadamu za Kimataifa na Utawala wa Makampuni, Chuo Kikuu cha Leeds, UK

Domimic ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi inayoitwa Open Mind Tanzania (OMT). OMT inajukumu la kuwawezesha vijana kuboresha ujuzi wao ili kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao. OMT hufanya uchechemuzi wa sera zinazohusu vijana ili ziweze kuchagiza maendeleo endelevu.

Badru Juma Rajabu
Mjumbe wa Bodi
Contact Info
Education
Shahada ya Sanaa katika Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda

Badru Juma Rajabu ni Mratibu Mwandamizi wa Programu wa Asasi ya Restless Development.  Restless Development ni Asasi inayoongozwa na vijana ambayo imekuwa akifanya kazi nchini Tanzania tangu 1993 ikiwa na rekodi ya kuvutia katika utendaji kazi wake unaoleta athari chanya kwa umma kwa kupitia programu za maendeleo zinazosimamiwa na vijana zinazoendana na Mipango ya Taifa ya Maendeleo.

Badru amefanya kazi UN Global Compact kama kiongozi wa programu inayohusika na uendelevu, ikisaidia biashara za Kitanzania kuoanisha mikakati na utendaji na kanuni za Kiulimwengu za Haki za Binadamu, kazi, na kupambana na rushwa, na kuchukua hatua zitakozofikia malengo ya jamii.