Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum mnamo tarehe 10/04/2013 ilikutana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Ofisi za THBUB. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama wa Policy Forum, Sekretariati ya Policy Forum na wafanyakazi wa THBUB.

Katika hotuba ya ufunguzi Mheshimiwa Bernadeta pamoja na mambo mengine alizungumzia dhumuni na malengo ya mkutano huo ukiwa ni pamoja na kuainisha namna ya ushirikiano baina ya Tume na Policy Forum pamoja na maeneo ya ushirikiano huu. Baada ya hotuba hiyo fupi alifungua Mkutano rasmi saa 09.00 asubuhi.

Baada ya ufunguzi huo, Bi Regina Mongi alitoa hotuba ya ukaribisho kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtandao wa Policy Forum, Bw. Audax Rukonge. Pamoja na mambo mengine Bi Regina aliushukuru uongozi wa THBUB kwa kuweza kuandaa mkutano huo ambao unatoa fursa ya jinsi pande hizi mbili zinaweza kushirikiana katika kuimarishwa kwa utawala bora na uzingatiwaji wa haki za binadamu. Pia kuweza kujua shughuli zifanywazo na pande hizi mbili.

Wajumbe walijulishwa juu ya kazi za pande zote mbili na walijadiliana kuhusiana na kazi zao na jinsi ambavyo wanaweza kufanya kazi pamoja.

Wajumbe walipendekeza maazimio mbalimbali ya namna ya kusonga mbele baada ya kikao hiki. Maazimio hayo ni pamoja na: Kuunda timu ndogo ya kiweza kuangalia jinsi PF na Tume inavyoweza kushikiana katika kutoa machapisho yahusuyo Haki za Binadamu na Utawala Bora, PF kushirikiana na Tume katika mijadala inayohusiana na Haki za Binadamu na Utawala Bora-hasa katika Breakfast Debates za kila mwezi zinazofanywa na PF, Kwa kuwa suala la elimu lilijitokeza sana katika mjadala, hivyo ilikubaliwa timu ya watu wachache kuomba rasimu ya Katiba mpya na kuijadili ili kuangalia suala la elimu katika katiba mpya limezungumziwaje, kuhusiana na upatikanaji wa taarifa na ushirikiano, tume wawe na mtu husika “contact person” kwa ajili ya mashirika ya kiraia, Tume kushirikisha wananchi katika kuishiwashi serikali kuyazingatia mapendekezo wanayoyatoa, Kuhusuiana na rasilimali fedha, ilipendekezwa kuwe na mkakati wa kufanya “fundraising” ya pamojaili kutatua changamoto ya rasilimali fedha na Kuundwa kwa “task force” wa ufuatiliaji