Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania - Mwongozo wa Jamii za Kiraia
Bajeti kwa kawaida imekuwa ikichukuliwa kuwa ni kazi ya wataalamu, wachumi na wahasibu tu. Lakini uamuzi wa Serikali wa namna gani ya kukusanya mapato huwaathiri wananchi wote. Kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi nyingine huathiri bei za vitu vinavyotumiwa katika kaya. Uamuzi wa matumizi ya serikali ndio huweka wazi iwapo viwango vya mishahara ya walimuna iwapo kutakuwa na dawa na vifaa vya kutosha katika zahanati au la.