Tamko Rasmi:-Bajeti 2015/2016
Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2015/16 kwa sasa inajadiliwa Bungeni. Bajeti nzima ya Serikali itawasilishwa na Waziri wa Fedha mara baada ya uwasilishaji na mjadala wa bajeti za wizara kukamilika. Kwa kuzingatia umuhimu wa tukio hili kitaifa, wajumbe wa Kikundi Kazi cha Bajeti cha Policy Forum, tunapenda kutoa mchango wetu katika mchakato huu muhimu kwa kuchangia uchambuzi wetu.