Zipo nyaraka nyingi zinazoonesha kuwa Tanzania imejaliwa madini mbalimbali yakiwamo almasi, dhahabu, na madini ya vito yasiyopatikana mahali pengine popote duniani, Tanzanite.
Hivi karibuni, sekta ya madini iliwekwa kwenye kipaumbele na Serikali ya Tanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchangia katika ukuaji wa haraka wa uchumi wa nchi.