Kuvuja kwa mkataba wa Statoil kunadhihirisha kuwa usiri unavunja imani
Kufuatia ugunduzi wa uhakika wa hivi karibuni wa gesi asilia Tanzania, nchi imejitokeza kuwa na uwezekano mkubwa wa uzalishaji gesi kwa kiwango cha juu katika Afrika ya Mashariki, na kuleta hamasa miongoni mwa wananchi, jumuiya za kiraia, na wanasiasa kuhusu matarajio ya rasilimali hiyo kuchochea maendeleo ya taifa . Serikali, inaaminika, imeanza mchakato wa kuandaa sera na miundo ya kisheria zitakazosaidia usimamizi wa uchunguzi, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia.