Skip to main content

Kwa nini afya siyo kipaumbele katika bajeti ya taifa 2011/12

Imechapishwa na Policy Forum

Mchakato wa bajeti ya mwaka unatoa fursa ya kutathmini kama taarifa kwa umma kuhusu vipaumbele vya serikali vinafuatwa. Kwa mfano, katika miaka ya hivi karibuni serikali imeonyesha nia ya kutaka kupata thamani halisi ya fedha kadri inavyotoa bajeti yake ili kuweza kukabiliana na matumizi yasiyo ya lazima. Uchambuzi huu wa bajeti ya sekta ya afya 2011/12 kwa ufupi unatoa malengo maalumu yanayo tathmini thamani ya fedha. Uchambuzi unapima jinsi rasilimali zilizopo zimeweza kugawanywa na kama mgawanyo huo utaweza kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.

Mgawanyo wa bajeti ya Sekta ya Kilimo: Je, nini hatma ya wakulima wadogo Tanzania?

Imechapishwa na Policy Forum

Kama sekta ya kilimoTanzania itawekezwa ipasavyo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Kwa mujibu wa taarifa ya bajeti 2011/12 iliyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya kilimo, kwa sasa sekta hii ina ajiri asilimia 77.5 ya watanzania na kuchangia asilimia 95 ya chakula kinachotumika nchini. Sekta ya kilimo pia inaonekana kukua kwa asilimia 4.2 tangu mwaka 2010 kutoka asilimia 3.2 ya mwaka uliotangulia.

Ijue Sheria Mpya ya Madini Namba 14 ya 2010

Imechapishwa na Policy Forum

Sheria hii mpya ya madini imetungwa baada ya mchakato mrefu uliotanguliwa na Kamati na tume mbalimbali zilizoundwa pamoja na msukumo mkubwa kutoka asasi za kiraia na kuhitimishwa na Tume iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani iliyoundwa mwaka 2007. Sheria hii inaweka utaratibu wa kisheria katika kutekeleza sera mpya ya madini ya mwaka 2009. Sheria hii ya madini namba 14 ya mwaka 2010 ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Aprili 2010 na kusainiwa na Rais tarehe 20 Mei, 2010.

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini

Imechapishwa na Policy Forum

Mwongozo huu umetolewa na Policy Forum katika jitihada zake za kurekodi yale yaliyojiri waliposhirikiana na wabunge katika kuchangia sheria mpya ya madini Tanzania, na kuboresha uwezo wa asasi za kiraia na vyombo vya habari katika kusimamia utendaji wa serikali kwenye sekta ya uziduaji (mafuta, gesi asilia na madini). Programu hii ilifanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Revenue Watch. Kusoma zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini. bofya hapa

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii (5th Edition, 2011)

Imechapishwa na Policy Forum

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi. Kwa maelezo zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini.

Tamko la Ngurdoto la Kamati ya Viongozi wa Dini na Asasi za Kiraia Oktoba 20, 2011

Imechapishwa na Policy Forum

Sisi, Kamati ya Viongozi wa Dini kwa Masuala ya Kijamii, Uchumi, Haki na Uhifadhi wa Mazingira na Maumbile na wanachama wa Policy Forum, tuliokutana katika Mkutano Mbadala wa masuala ya Madini mjini Arusha tarehe 20 Oktoba 2011, tumejadili kwa kina madhara yatokanayo na shughuli za uchimbaji wa madini katika jamii zionazoishi karibu na migodi ya madini na kwa mazingira, na tunaiomba serikali na Bunge kuhakikisha kuwa zinatekeleza kwa dhati majukumu yao kwa kuhakikisha kuwa haki za wananchi ambao hawajanufaika na shughuli za uchimbaji wa madini licha ya shughuli hizo kuwadhulumu ardhi

Policy Forum Kushiriki katika semina ya asubuhi ya ukwepaji haramu wa mitaji katika nchi maskini iliyofanyika sweden

Imechapishwa na Policy Forum

Moses Kulaba, Mwakilishi wa kikundi kazi cha bajeti akiwa anatoa mada Stockholm tarehe 23 Septemba                                                       

Tarehe 23 Septemba kikundi kazi cha Bajeti(BWG) cha Policy Forum  kilialikwa na Forum Syd na Svenska Institutet kutoa neno katika semina ya asubuhi iliyohusu ukwepaji haramu wa mitaji katika nchi maskini, jinsi gani inaathiri maendeleo, na jinsi gani inaweza kusimamishwa.               

Mada ilitoka katikati ripoti mpya ambayo Kikundi kazi cha bajeti cha Policy Forum kilikuwa mwandishi mwenza.

Subscribe to Resources