Habari

Ijue Sheria Mpya ya Madini Namba 14 ya 2010

Sheria hii mpya ya madini imetungwa baada ya mchakato mrefu uliotanguliwa na Kamati na tume mbalimbali zilizoundwa pamoja na msukumo mkubwa kutoka asasi za kiraia na kuhitimishwa na Tume iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani iliyoundwa mwaka 2007. Sheria hii inaweka utaratibu wa kisheria katika kutekeleza sera mpya ya madini ya mwaka 2009. Sheria hii ya madini namba 14 ya mwaka 2010 ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Aprili 2010 na kusainiwa na Rais tarehe 20 Mei, 2010.

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini

Mwongozo huu umetolewa na Policy Forum katika jitihada zake za kurekodi yale yaliyojiri waliposhirikiana na wabunge katika kuchangia sheria mpya ya madini Tanzania, na kuboresha uwezo wa asasi za kiraia na vyombo vya habari katika kusimamia utendaji wa serikali kwenye sekta ya uziduaji (mafuta, gesi asilia na madini). Programu hii ilifanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Revenue Watch. Kusoma zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini. bofya hapa

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii (5th Edition, 2011)

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi. Kwa maelezo zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini.

Tangazo la Policy Forum la Uwazi na Uziduaji katika Sekta ya Madini

Categoriest

Policy Forum imetoa tangazo juu ya Sekta ya nishati na madini Tanzania ambalo kwa sasa linarushwa hewani katika vituo viwili vya Televisheni ambavyo ni ITV na Star TV. Lengo la tangazo ni kuwafanya raia wa kawaida wa Tanzania kuuliza viongozi wao juu ya rasilimali ya madini yao ambayo inapaswa kutumiwa kwa manufaa ya watanzania na si vinginevyo. Ona tangazo chini 

Tamko La Ngurdoto La Kamati Ya Viongozi Wa Dini Na Asasi Za Kiraia Oktoba 20, 2011

Categoriest

Sisi, Kamati ya Viongozi wa Dini kwa Masuala ya Kijamii, Uchumi, Haki na Uhifadhi wa Mazingira na Maumbile na wanachama wa Policy Forum, tuliokutana katika Mkutano Mbadala wa masuala ya Madini mjini Arusha tarehe 20 Oktoba 2011, tumejadili kwa kina madhara yatokanayo na shughuli za uchimbaji wa madini katika jamii zionazoishi karibu na migodi ya madini na kwa mazingira, na tunaiomba serikali na Bunge kuhakikisha kuwa zinatekeleza kwa dhati majukumu

Tamko la Ngurdoto la Kamati ya Viongozi wa Dini na Asasi za Kiraia Oktoba 20, 2011

Categoriest

Sisi, Kamati ya Viongozi wa Dini kwa Masuala ya Kijamii, Uchumi, Haki na Uhifadhi wa Mazingira na Maumbile na wanachama wa Policy Forum, tuliokutana katika Mkutano Mbadala wa masuala ya Madini mjini Arusha tarehe 20 Oktoba 2011, tumejadili kwa kina madhara yatokanayo na shughuli za uchimbaji wa madini katika jamii zionazoishi karibu na migodi ya madini na kwa mazingira, na tunaiomba serikali na Bunge kuhakikisha kuwa zinatekeleza kwa dhati majukumu yao kwa kuhakikisha kuwa haki za wananchi ambao hawajanufaika na s

Pages

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter