Skip to main content

Tathmini wa Usimamizi wa rasilimali kwa Mwaka 2013

Imechapishwa na Policy Forum

Uchimbaji madini huchangia asilimia 5 ya pato ghafi la ndani na theluthi moja ya mauzo ya nje.. Mwaka 2011 thamani ya mauzo ya nje ya madini ilifikia kiasi cha dola za marekani bilioni 2.1, kati ya hizo zaidi ya asilimia 95 zilitoka katika machimbo sita ya dhahabu. Tanzaniapia inazalisha shaba, madini fedha, almasi, na gesi asilia. kusoma soma kiambatanisho hapa chini

Ujumbe kutoka Tanzania kwa Obama: Uwazi hujenga taasisi yenye nguvu

Imechapishwa na Policy Forum

Rais wa Marekani Barack Obama na vyombo vya habari wanaweza kusafiri kuja katika nchi yangu wiki hii kwa majadiliano juu ya masuala  ya 'mvuto' kama  ya ushindani wa kiuchumi wa  Marekani na China au amani na masuala ya usalama. Hata hivyo kama   kweli Marekani  ipo makini kuhusu kusukuma utawala wa kidemokrasia duniani kote, ni  mambo  haya madogo ya 'mvuto'  ambayo ni muhimu zaidi.

Maoni ya Asasi za Kiraia Kuhusiana na Rasimu ya Sera ya Gesi

Imechapishwa na Policy Forum

Sisi, Asasi za kiraia awali ya yote tunapenda kwanza kuipongeza serikali yetu ya Tanzania kwa kufikia hatua ya kutengeneza rasimu ya sera ya Gesi Asilia iliyotolewa hivi karibuni. Hii imedhihirishwa kwetu kuwa serikali yetu inadhamira ya dhati katika kuhakikisha kuwa rasilimali ya Gesi inawanufaisha watanzania wote na kuchangia maendeleo katika nchi yetu.

Documentary ya Miaka Kumi ya Policy Forum ya Ushawishi na Utetezi wa Sera

Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum imeadhimisha miaka yake kumi ya ushawishi na uchechemuzi wa sera tokea ianze rasmi mwaka 2003, maadhimisho hayo yalifanyika katika mkutano wake mkuu wa mwaka pamoja na wanachama wake.

wanachama hao walionyeshwa documentary fupi inayoonyesha historia ya Policy Forum tokea ianze, changamoto ilizopitia na jinsi ambavyo ilikumbana na hizo changamoto, baada ya hapo baadhi ya wanachama wa Policy Forum  walieleza jinsi ambavyo wamefaidika kwenye mtandao huo.

Kuona documentary hiyo tafadhali bofya hapa

Tamko La Kikundi Kazi Cha Bajeti Cha Policy Forum Juu Ya Taarifa Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Serikali (Cag) Ya Mwaka 2011/2012

Imechapishwa na Policy Forum

Juma lililopita, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) aliwasilisha Bungeni taarifa yake ya  mwaka kuhusu mahesabu ya serikali kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2012 kufuatana na ibara ya 143  ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 34 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na: 11 ya mwaka 2008.  Taarifa inaonyesha baadhi ya masuala ambayo yanazuia ufanisi wa Serikali kuu, Serikali za mitaa, Mamlaka za umma na vyombo vingine kufikia malengo yao.

Policy Forum Yafanya Mkutano na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)

Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum mnamo tarehe 10/04/2013 ilikutana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Ofisi za THBUB. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama wa Policy Forum, Sekretariati ya Policy Forum na wafanyakazi wa THBUB.

Katika hotuba ya ufunguzi Mheshimiwa Bernadeta pamoja na mambo mengine alizungumzia dhumuni na malengo ya mkutano huo ukiwa ni pamoja na kuainisha namna ya ushirikiano baina ya Tume na Policy Forum pamoja na maeneo ya ushirikiano huu. Baada ya hotuba hiyo fupi alifungua Mkutano rasmi saa 09.00 asubuhi.

Toleo la Bajeti ya Mwananchi lilitolewa na Wizara ya Fedha ikishirikiana na Policy Forum

Imechapishwa na Policy Forum

Ni muhimu kila mwananchi kuuelewa na kushiriki katika mchakato mzima wa kutengeneza bajeti ya nchi yao kwahiyo basi ni vema hawa wananchi kupewa taarifa/habari za kutosha.

Kwasababu hii basi Policy Forum imekuwa ikitoa kijitabu kidogo kinachoonyesha bajeti ya nchi ya miaka husika.

Mheshimiwa Likwelile katika Mdahalo wa Policy Forum wa Juni 2010 aliahidi kuwa serikali itakuwa ikitoa vijitabu hivyo vinavyoelezea bajeti husika ili mwananchi wa kawaida aweze kuelewa.

Katiba Mpya na Ufanisi wa Serikali za Mitaa Tanzania

Imechapishwa na Policy Forum

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni katiba iliyotungwa mwaka 1977. Katiba hii inaielezea Tanzania kama nchi ya kidemokrasia, inayofuata misingi na haki za binadamu na siasa yake ni ya vyama vingi. Katiba ni sheria mama ya nchi inayowawezesha wananchi kujitambua kama taifa na ya kiutawala inayoelezea mgawanyo wa madaraka na majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola.

Subscribe to Resources