Tangazo la Kifo: Mungu Akulaze Mahali Pema Peponi Alex Modest Ruchyahinduru
Sekretariati ya Policy Forum inasikitika kutangaza kifo cha Alex Modest Ruchyahinduru, meneja wetu wa Mawasiliano na Uchechemuzi, aliyefariki asubuhi ya leo Mei Mosi 2016 katika hospitali ya Aga Khan mjini Dar es Salaam. Baadhi yenu huenda mlikuwa na taarifa za kulazwa kwake kufuatia operesheni ya kichwa iliyofanyika kipindi cha Pasaka takriban mwezi mmoja uliyopita. Alex alijiunga na Policy Forum Machi 2009.