Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Kwa: Mawaziri wa Fedha wa Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kenya, Jamhuri ya Rwanda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda.

YAHUSU: Kukomesha Misamaha ya Kodi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki

Katika siku ya leo ambayo tunaadhimisha Siku ya Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 30 Novemba 2013, sisi, Mashirika ya kiraia kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tunapenda kutoa tamko na kutaka kuchukuliwa hatua ya dharura ya kukomesha misamaha ya kodi ili kuweza kuboresha hali ya maisha ya wananchi. Katika siku hii, ambayo inalenga kuimarisha na kukuza umoja Afrika Mashariki, tunapenda kutoa wito wa dhati kwa Mawaziri wa Fedha wa Afrika mashariki watumie siku hii ya leo kuonyesha mfano kwa mataifa mengine ya afrika, kwa kuwa mstari wa mbele kufunga mianya ya sheria inayosababisha ukwepaji kodi na kukomesha misamaha ya kodi isiyokuwa na tija kwa taifa.

Mapato yaliyopotea katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Kupitia Misamaha ya Kodi.

Serikali za Afrika Mashariki zinatoa misamaha mbalimbali ya kodi kama motisha kwa wafanyabiashara ili kuvutia zaidi viwango vya uwekezaji wa kigeni, kwa lugha ya kingereza uwekezaji huo unaitwa ‘Foreign Direct Investments’ (FDI). Misamaha  hiyo ni pamoja na kusamehewa  kodi ya mapato ya kampuni hasa katika sera ambayo inatenga maeneo maalum kwa uwekezaji (EPZs), na kupunguza kutoka kiwango cha kawaida ya kodi kama vile ushuru wa forodha na kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Hata hivyo ushahidi unaonyesha kuwa misamaha hiyo ya kodi inaipotezea serikali mapato na pia misamaha si muhimu ili kuvutia wawekezaji Afrika Mashariki. Kwa ujumla, Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda kwa pamoja inapoteza hadi dola bilioni 2.8 kwa mwaka kwa kupitia misamaha ya kodi inayotolewa ili kumpa motisha mwekezaji. Hii ni fedha inayoweza kugharamia huduma za umma, kuboresha maisha ya wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kupunguza umaskini na kuleta usawa katika kanda.

Biashara kubwa, na Ambazo Hazilipiwi Kodi.

Wakati makampuni makubwa ya kimataifa yanapokea motisha wa misamaha ya kodi, na kwa sababu hiyo hawalipi kodi ambayo ni haki ya kila mfanyabiashara, wananchi mwisho wa siku ndio wanaobeba mzigo mkubwa wa kodi kwa kupitia kodi inayolipwa kutoka kwenye mishahara (PAYE) na kodi ambayo mwananchi analipa kila siku kwa kununua bidhaa (VAT). Kwa sababu hiyo, maisha ya mwananchi wa Afrika Mashariki yanazidi kuwa ya gharama kubwa zaidi, umaskini unaongezeka, ukosefu wa usawa umekuwa mbaya zaidi. Wakati nchi husika zikipigania  kupanua wigo wa kodi ili kuongeza mapato ya ndani, wananchi maskini hawapaswi kuongezewa mzigo wa maisha. Mapato yaliyopotea kwa misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa ya uwekezaji, yangeweza kwa kiasi kikubwa kupunguza umaskini kwa kuboresha huduma za jamii.

 

Ukomeshaji wa Misamaha ya Kodi Unawezekana

Hakuna sababu kwa nini makampuni haya lazima yaendelee kupokea misamaha ya kodi ambayo inapunguza mapato ya nchi na hatimae kuwanyima haki wananchi ya kupata huduma bora za kijamii.

Matokeo ya utafiti yaliyofanywa na Benki ya Dunia na Taasisi ya Fedha ya Kimataifa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kubaini ni mambo gani ambayo yanavutia wawekezaji, inaonyesha kwamba wawekezaji hawawekezi Afrika Mashariki kwa sababu ya kupewa misamaha ya kodi, kinachowafanya wawekeze Afrika Mashariki ni pamoja na kuwepo miundombinu, uwepo wa utulivu na amani, uwepo wa rasilimali watu na upatikanaji rahisi wa masoko.

Afrika Mashariki Ionyeshe Mfano kuto-toa Misamaha Ambayo Siyo ya Lazima

Tunakaribisha na tunaunga mkono hatua mbalimbali za mapendekezo katika Kanuni za Maadili dhidi ya misamaha ya Kodi inayopendekezwa na jumuisho la Afrika Mashariki. Hatua hii itapunguza ushindani wa kodi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuongeza uwazi na kubadilishana habari juu ya misamaha ya kodi ,na kupitisha sera inayopinga uhamisho wa bei, kwa lugha ya kigeni inaitwa ‘Transfer pricing’.

Hata hivyo, upitishwaji wa kanuni hiyo inayohusu misamaha ya kodi inahitajika kwa nguvu zote kwani kumekuwa na kusubiri kwa muda mrefu kwa nchi wanachama kuridhia suala hilo. Kunahitajika utashi wa kisiasa kuhakikisha kanuni inapita, pia kunahitajika sheria kwa nchi wanachama ambayo itaifanya kanuni hiyo iweze kuwa na nguvu ya kisheria. Pia tunatoa changamoto kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na taratibu ya kuchambua masuala ya kodi na kuifanya kama sehemu ya kawaida ya mchakato wa bajeti.

Ili kuzuia mashindano ya kodi kuelekea chini (Race to the Bottom) katika kanda,  badala yake kuhakikisha kwamba Umoja wa Afrika Mashariki unajikita kukuza uchumi na usawa katika jamii. Tunaitaka Afrika Mashariki  kuweka mfano kwa kuongoza katika mchakato wa kukomesha misamaha ya kodi kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Maadili dhidi ya misamaha ya Kodi ya Ushindani katika Jumuiya ya Afrika Mashariki .

Kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu kanuni za maadili ya misamaha ya kodi, Jumuiya ya Afrika Mashariki ina wajibu kwa raia wake wa kuoanisha misamaha ya kodi katika kanda kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi wa mgao wa rasilimali ndani ya Jumuiya. Mkataba  huo wa kanuni za maadili kuhusu misamaha ya kodi pia unaonyesha nia ya kuimarisha soko la pamoja kwa kuondoa mashindano ya misamaha ya kodi yasiyokuwa ya lazima. Kwa kutambua hayo, tunatoa wito kwa , Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki , kuonyesha nia na kuwa mstari wa mbele barani Afrika kwa kuchukua hatua madhubuti kukomesha misamaha ya kodi yenye madhara  kwa kusaini Kanuni za Maadili dhidi ya madhara ya Kodi ya Ushindani katika Afrika Mashariki.

Imesainiwa na:

East African Tax and Governance Network (EATGN)Kenya (Network of over 16 member organizations geared towards establishing a vibrant tax justice movement across the Eastern Africa region that mobilizes citizen participation in influencing policy and practice for a just and equitable society.)

Policy ForumTanzania (Over 100 non-governmental organizations registered in Tanzania, drawn together by specific interest in influencing policy processes to enhance poverty reduction, equity and democratization.)

Southern and Eastern African Trade Information and Negotiations Institute (SEATINI)Uganda (An African initiative to strengthen Africa's capacity to take a more effective part in the emerging global trading system and to better manage the process of Globalization.)

PARCEM, “Parole et Action pour le Réveil des Consciences et l'Evolution des Mentalités”, (Speech andActionfor theConsciousnessRaising andtheEvolution ofMentalities) a National civil Society organization engaged in advocacy for democratic governance, accountability and transparence and civic education

OAG (Observatory of Governmental Action), Burundi civic rights groups of 18 associations, parliamentarians and journalists

OLUCOME, the Observatory on Anti-corruption and Economic Malpractice, counting 7000 members and working in the all provinces of Burundi

SYGECO (Syndicat Général des Commerçants du Burundi(General Trade union of Burundi Traders), the most representative trade Union of small business sector with 5000 active members,

CONAPES (Conseil National du Personnel de l’Enseignement Secondaire ), the National Council  of Secondary Education Cycle workers, representing 5000 members and working across all the 17 provinces of Burundi

SYNAPA (Syndicat National du Personnel Paramedical et Aide-Soignants), the National Trade Union of Paramedical Staff and Caregivers, representing 6000 members et working in all the 17 provinces of Burundi

FOCODE (Forum pour la Conscience et le Développement), the Forum Conscience Raising and Development, representing 1800 members et working across 6 provinces of Burundi