Usawa wa Kodi Mwongozo wa mafunzo kwa Tanzania
Mifumo ya kodi ni msingi kwa maendeleo ya usawa kwa taifa lolote, inabeba nafasi muhimu katika kuhamasisha rasilimali na kutoa huduma muhimu. Hata hivyo, katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania, ukosefu wa usawa kimfumo mara nyingi huzuia mifumo hii kufikia usawa na ushirikishwaji. Makundi yaliyotengwa, ikiwa ni pamoja na kaya za kipato cha chini na wanawake mara nyingi hubeba mzigo wa kodi usio na uwiano, ilhali faida za mapato ya umma hazijagawanywa kwa usawa.