Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Serikali ya Tanzania inatoa wigo mpana wa motisha wa kodi kwa wafanya biashara ili kuvutia viwango vikubwa zaidi vya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDIs) nchini.

Utoaji wa motisha ya kodi Tanzania, tunaweza kusema ni sehemu ya ushindani wa kodi miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC). Kufuatia uundaji wa EAC mwaka 1999, Kenya, Tanzania, na Uganda walianzisha umoja wa forodha (eneo ambalo halina ushuru wa forodha na lenye kiwango cha tozo ya bidhaa zinazotoka nje ya nchi kinachofanana) mwaka 2005, na Rwanda na Burundi wakajiunga mwaka 2009.

Hali hii imejenga eneo pana zaidi kikanda kwa uwekezaji wa moja kwa moja toka nje (FDIs) kwa ujumla hususan kwa uwekezaji-utafutaji masoko. Chini ya soko la pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki, mashirika ya kibiashara kwa ujumla na hasa mashirika ya biashara za kimataifa yanayojihusisha na uwekezaji wa nje yanaweza kuwekeza popote ndani ya nchi wanachama.

Wakati huo huo lakini, nchi zinashawishika kuongeza motisha ya kodi kuvutia uwekezaji wa nje endelevu ili kunufaika kutokana na huu uwekezaji kwa njia ya ajira, mapato kutokana na kodi, ada, mrabaha na gawio kati ya nyinginezo; mfungamano wa kisekta; uhamishaji wa kiteknolojia, na faida nyingine zinazowezekana kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa uchumi wa nchi wanazowekeza.

Uchambuzi wetu unaonesha kuwa utoaji wa motisha ya kodi katika Kanda ya Afrika ya Mashariki kwa ujumla na hasa nchini Tanzania unaonesha ushindani wa kodi wenye madhara na unaweza kuwa ‘mbio za kuelekea chini’.

Bofya hapa kusoma zaidi.