Tamko La Policy Forum : Bajeti Ya 2017/18: Mamlaka Na Ufanisi Wa Serikali Za Mitaa
Sisi wanachama wa Policy Forum, Mtandao wa Asasi za Kiraia;
Kufuatia kupitishwa kwa bajeti ya mwaka 2017/18 na Bunge la Bajeti la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) Juni 2017;
Kwa kuzingatia juhudi dhahiri za Serikali ya JMT katika kuongeza ukusanyaji wa mapato ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za mandeleo kwa Watanzania;