Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Sekretariati ya Policy Forum inasikitika  kutangaza kifo cha Alex Modest Ruchyahinduru, meneja wetu wa Mawasiliano na Uchechemuzi, aliyefariki asubuhi ya leo Mei Mosi 2016 katika hospitali ya Aga Khan mjini Dar es Salaam. Baadhi yenu huenda mlikuwa na taarifa za kulazwa kwake kufuatia operesheni ya kichwa iliyofanyika kipindi cha Pasaka takriban mwezi mmoja uliyopita. Alex alijiunga na Policy Forum Machi 2009.

Mipango ya mazishi inaendelea na tutawajulisha kadri tunavyowasiliana na familia ya marehemu. Kwa wanachama wenye salamu za rambirambi, tafadhali tumeni kwa njia ya barua pepe: info@policyforum.or.tz na tutazifikisha kwa familia yake.

Alex ameacha mjane na watoto wawili wa kike.

Tulimpenda katika uhai wake, tusimsahau bada ya mauti.