Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini: Mfumo wa Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG)
Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya tathmini ya mwaka na ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa shughuli zinazogharamiwa na Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG) kama zinavyotekelezwa mara kwa mara na Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Uhusiano huu unatokana na ukweli kwamba ufuatiliaji unaopaswa kufanywa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa unagusa kwa kiwango kikubwa masuala yaleyale au maeneo muhimu ambayo hufanyiwa tathmini wakati wa upimaji wa mwaka.