Skip to main content

Tamko la asasi za kiraia

Imechapishwa na Policy Forum

TAARIFA YA ASASI ZA KIRAIA KWA UMMA KUHUSU KUFUTWA KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012; 07 Mei 2013 Tarehe 03 Mei 2013, serikali ilitangaza Bungeni kuwa imeyafuta matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2012 ili yafanyiwe maboresho (standardization) na baadaye kupangwa upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Akiwasilisha tamko la serikali bungeni, Mh.

Muongozo kuhusu muundo, utaratibu wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya Katiba ya wilaya

Imechapishwa na Policy Forum

Kwa mujibu wa Kifungu cha 18 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83, Tume inawajibu wa kuunda Mabaraza ya Katiba kwa ajili ya kupitia na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume. Muundo wa Mabaraza ya Katiba unapaswa kuzingatia mgawanyiko wa kijiografia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mabaraza ya Katiba yatawashirikisha na kuwakutanisha wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii kwa lengo la kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba.

HAKI ZA MAZINGIRA, UHIFADHI NA UTUNZAJI MAZINGIRA TANZANIA:UHALALI WA KUINGIZWA KWAKE KATIKA ITAKAYOKUWA KATIBA MPYA

Imechapishwa na Policy Forum

Mada hii inalenga katika kuchochea mjadala na kutoa taarifa zaidi katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Inatoa majumuisho (usanisi) ya mapitio ya katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba za baadhi ya nchi zilizochaguliwa ambazo zimezingatia haki za mazingira, uhifadhi na menejimenti yake. Mapitio hayo yanadokeza uingizaji wa vipengele vya haki za mazingira, uhifadhi na manejimenti yake katika itakayokuwa - katiba mpya. Mada hii inatoa mapitio na mapendekezo juu ya nini kifanyike ili kuhakikisha kuwa

Mwongozo wa Katiba kwa Raia (toleo la tatu)

Imechapishwa na Policy Forum

Nchi yetu iko kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya. Katiba iliyopo iliachwa na wakoloni waingereza ili itumike kwa muda wakati Katiba ya kudumu ikiandaliwa na watanzania wenyewe. Matarajio ya kuweza kuandaa mchakato wa kupata Katiba ya watanzania wenyewe hayajawahi kufanikiwa.

Mazungumzo Ya Asasi Za Kiraia Juu Ya Ukwepaji Haramu Wa Fedha Afrika

Imechapishwa na Policy Forum

Wiki hii Policy Forum ilifanya mjadala maalum wa nusu siku kuhusiana na ukwepaji haramu wa fedha kutoka Afrika na wataalamu wawili wa kimataifa wa mada hii ambao ni Baker Raymond, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Financial Intergrity,taasisi inayoongoza ya kimataifa ya uchunguzi wa fedha haramu  uliounganishwa na Alvin Mosioma, Mratibu wa Tax Justice Network Afrika, taasisi ambayo ina lengo la kukuza haki za kijamii,

Taarifa Ya Umma Inayohusu Kukamatwa Kwa Wanaharakati Wa Haki Za Binadamu

Imechapishwa na Policy Forum

Mtandao wa Watetezi wa  Haki za Binadamu Tanzania (THRD-Coalition) unaoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Pamoja na mtandao wa asasi za kiraia wa Policy Forum wanatoa wito kwa Serikali kuwaachia mara moja Watetezi wa  haki za binadamu 16 ambao waliwekwa chini ya ulinzi mnano tarehe 9/2/2012 katika eneo la Hospitali ya Tai

Utambulisho Wa Filamu Ya Kijiji Cha Tambua Haki

Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum kwa kushirikiana na Kanumba the Great Films wanayo furaha kuitambulisha kwenu filamu ya Kijiji cha Tambua Haki, filamu ambayo ina lenga kuelimisha jamii juu ya utawala bora na uwajibikaji katika ngazi ya serikali za mitaa hadi kitaifa.Utambulisho huu ulifanywa tarehe 8 Februari 2012 katika hoteli ya Regenct Park.

Majadiliano Juu Ya Nafasi Ya Mazingira Na Maliasili Katika Katiba Mpya Ya Tanzania

Imechapishwa na Policy Forum

Tanzania inaelekea kipindi cha marekebisho ya kihistoria ya katiba yake, mchakato umeshika kasi kubwa baada ya uchaguzi mkuu wa 2010. mchakato wa marekebisho haya yanayoendelea kwa kiasi kikubwa umeweka mbele masuala ya kupunguza nguvu za rais, haja ya kubadili Tume ya Taifa ya Uchaguzi, suala la haja kwa wagombea binafsi, na uchaguzi huru na wa haki.

Subscribe to Resources