Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tunakuletea tena chapisho hili la pili katika mtiririko wa machapisho yanayohusu elimu kwa umma juu ya kupambana na rushwa. Mtakumbuka kuwa chapisho letu la kwanza la pamoja lilihusu sheria mpya namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa hapa Tanzania, Chapisho hili linaweka wazi sheria zetu zinavyosema kuhusu makosa ya rushwa katika chaguzi hapa nchini Tanzania na adhabu zinazotolewa kwa makosa husika, Kwa kuzingatia kuwa tutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2009 na Uchaguzi Mkuu 2010 tunaamini chapisho hili litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wakati wa chaguzi zetu hizi mbili muhimu.

Katika chapisho hili tumekusudia kuweka anwani na simu za ofisi zote za mikoa na Wilaya za TAKUKURU ili kuwarahisishia wananchi kuweza kuwasiliana na ofisi hizi pale tatizo lolote linapojitokeza. Ni matumaini yetu kuwa mchakato ulioanzishwa na serikali wa kutunga sheria zingine kama sheria ya uhuru wa habari (Freedom of Information Act), ya vyombo vya habari (Media Services Act) na ile ya kuwalinda watoa taarifa (Whistle Blowers Protection Act) utaongeza nguvu na kasi katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania. Kusoma zaidi bofya hapa