Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la madai ya uwajibikaji kutoka kwa Wabunge ambayo yamebadilisha muonekano wa Bunge na yamepelekea kujiuzuru kwa mawaziri kadhaa, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu. Mswada wa Sheria ya Ukaguzi imepelekwa Bungeni chini ya hati ya dharura na itajadiliwa katika kikao kijacho cha Bajeti mwaka huu. Mswada huu unalenga kuiongezea Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAO) uhuru mkubwa wa kutoingiliwa na Dola katika utendaji wake wa kumsaidia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Watanzania watakuwa wanafuatilia kwa karibu kuona iwapo mswada huo utaongeza uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.

Endelea.