Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum kwa kushirikiana na Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta Tanzania ( TEITI ) pamoja na Hakimadini wameandaa warsha ( 2-3 Aprili 2014) Arusha kwa lengo la kuwawezesha wawakilishi wa asasi za kiraia za kaskazini mwa Tanzania zinazofanya kazi katika masuala ya uziduaji kuongeza uelewa wao wa viwango vipya vya  Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini au Mpango wa Uwazi katika Tasnia ya Uziduaji (EITI) ili kuongeza uwezo wao wa kuiwajibisha serikali yao.

Bi Alice Swai kutoka sekretariati ya TEITI aliwatambulisha washiriki katika Viwango vipya vya EITI vilivyoundwa mwaka 2013. Alisema kwamba viwango hivi viliundwa baada kubaini kuwa viwango vya 2011 vinalenga hasa kukuza uwazi katika mapato yanayotokana na sekta ya madini ( hasa katika masuala ya ukusanyaji wa kodi ) lakini ilijikita kidogo katika kuongeza uwazi katika maudhui ya mikataba ya sekta ya madini . Alisema ilionekana vema kuiimarisha EITI ili kufikia kiwango cha Open Government Partnership ( OGP ) ambao ina lengo la kukuza uwazi wa serikali si tu katika masuala yanayohusiana na bajeti, lakini ni pamoja na mikataba ya serikali inayoingia na sekta binafsi.

Viwango vipya vya 2013 vinahamasisha kutoa taarifa ya leseni na mikataba ikiwa pamoja na ile mikataba ambayo nchi huingia na nchi nyingine , alisema.

Bi Swai , alisema viwango vingine ni : kiwango cha juu ya kile kinachozalishwa na kile kinacholipwa (Ufuatiliaji wa Uzalishaji) ; uwazi katika ukusanyaji wa kodi na usambazaji mapato; uwazi wa usimamizi wa matumizi kwa maana kwamba ni lazima kuwa wazi kuhusiana na mapato yanayopatikana kutoka sekta ya madini na jinsi mapato hayo yanatumika kuchangia katika maendeleo ya nchi kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Alisema kuwa Tanzania inahitaji kwenda zaidi ya viwango hivi kwasababu sio viwango hivi peke yake ndio hupelekea utawala bora. "Kama asasi za kiraia tunapaswa kuwa na uwezo wa kuiwajibisha serikali yetu ili waweze kuwajibika kuanzia ngazi ya chini ambako wananchi wengi wapo katika njia sahihi ," alisema , akisisitiza kuwa uwazi peke yake katika sekta ya madini hautoshi bali ni lazima kuwepo na utawala bora na uwajibikaji .

Mheshimiwa Silas Olang kutoka Revenue Watch Institute ( RWI ) alisisitiza kuwa taarifa za EITI zinapaswa kuangaliwa kama taarifa ambazo zinaweza kuleta mabadiliko, alisema kuwa elimu juu ya uziduaji lazima isambazwe kwa wananchi kama ilivyoainishwa chini ya kanuni ya 4 ya EITI ambayo inatambua kwamba " uelewa wa umma juu ya mapato na matumizi ya serikali unaweza kusaidia mijadala ya umma na kupelekea kuchagua sera sahihi kwa ajili ya maendeleo endelevu. "Wananchi wanapopata taarifa, aliongeza,  wanakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa maoni yao na kushiriki katika uundaji wa sera ya sekta. Alifafanua zaidi kuwa hata lengo la mafunzo hayo  pia ni sehemu ya jitihada za kuwawezesha asasi za kiraia kupata uelewa sahihi ili kuleta mabadiliko ya sera.

Mwisho, alizungumzia  Tathmini ya Usimamizi wa Rasilimali ( RGI ) ambayo alisema hutumika kupima utendaji wa utawala katika sekta ya madini, na kubainisha kuwa nchi zinaweza pia kutumia tathmini hii kutambua maeneo ya kipaumbele kwa ajili ya