Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Zipo nyaraka nyingi zinazoonesha kuwa Tanzania imejaliwa madini mbalimbali yakiwamo almasi, dhahabu, na madini ya vito yasiyopatikana mahali pengine popote duniani, Tanzanite.

Hivi karibuni, sekta ya madini iliwekwa kwenye kipaumbele na Serikali ya Tanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchangia katika ukuaji wa haraka wa uchumi wa nchi.

Kutokana na malengo hayo na katika muktadha mpana wa mageuzi ya kisheria yanayolenga kuleta uchumi huria (kutokana na imani kuwa uchumi unaoongozwa kwa nguvu ya soko una uwezo wa kuleta maendeleo endelevu), Oktoba 1997, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini ilitoa rasmi Sera ya Sekta ya Madini. Sera hii ina lengo la kuongoza maendeleo na uvunaji wa madini nchini. Sheria ya Madini, 1998 (kama ilivyorekebishwa) imekuwa sheria kuu na inayoainisha mambo mengi kuhusu sekta hii ambayo inaifuata na, pamoja na mambo mengine, kuwa mbadala wa Sheria ya Madini, 1979. Sheria hii ilianza kutumika Julai mosi, 1999.

ENDELEA