Skip to main content

Warsha Ya Uwajibikaji Jamii Katika Mkoa Wa Mwanza

Imechapishwa na Policy Forum

Ikishirikiana na Mwanza Policy Initiative (MPI), wiki hii Policy Forum inaendesha warsha kuhusu Uwajibikaji Jamii (Social Accountability Monitoring – au kwa kifupi, SAM) kwa ajili ya asasi za kiraia za Mwanza.

PF Yaendeleza Ushirikiano Na Ofisi Ya Bunge

Imechapishwa na Policy Forum

Ile dhamira ya Policy Forum kushirikiana na Ofisi ya Bunge mwaka huu wa 2008 imeanza kutekelezwa kwa mfululizo wa vikao vya pamoja na wabunge, maafisa wa ofisi ya bunge na wana-ASASI.

Kikundi Kazi Cha Serikali Za Mitaa Chachapisha Tafsiri Rahisi Ya Kanuni Za Utawala Kijijini

Imechapishwa na Policy Forum

Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum (LGWG) kimechapisha tafsiri rahisi ya kanuni za utawala kijijini. Kitabu hicho kinachoitwa 'UTAWALA WA KIDEMOKRASIA KATIKA JAMII: USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA SERIKALI ZA MITAA (VITONGOJI, VIJIJI NA MITAA)', kinalenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mipango ya maendeleo katika vijiji na mitaa.

Warsha Kuhusu Mpango Wa Kurekebisha Serikali Za Mitaa - Ripoti Ya Awali

Imechapishwa na Policy Forum

Tarehe 26 na 27 Novemba 2007, Kikundi-kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum ikisaidiwa na Leadership Forum, kiliandaa warsha kuhusu mwelekeo wa Programu ya Kurekebisha Serikali za Mitaa kilichofanyika mji wa Kibaha. Dhumuni kuu lilikuwa kuwapa fursa maafisa wa TAMISEMI kutoa taarifa kwa wadau kutoka asasi mbalimbali kuhusu maendeleo ya programu hiyo.

Mkutano Wa Ufuatiliaji Matumizi Ya Fedha Za Umma Afrika Mashariki

Imechapishwa na Policy Forum

Katika miaka kumi iliyopita, asasi za kiraia katika nchi zaidi ya 60 duniani zimeanzisha mikakati ya kuchunguza jinsi serikali zao zinavyotumia pesa za umma. Harakati hizi zimefikia kuangalia kila hatua katika ya mchakato wa bajeti: mipango, utengaji wa mafungu, matumizi na matokeo ya matumizi. 

Subscribe to Resources