Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum tunayo furaha kuchapisha kitabu hiki ambacho kinatokana na ‘Taarifa ya Kamati ya Rais ya Kuishauri Serikali Kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini’ Juzuu Namba 2.

Shukrani kwa Reginald Martin wa LHRC kwa ushirikiano wake wa hali na mali ikiwa ni pamoja na kutumia muda wake kuhakikisha anaihariri Taarifa hii fupi. Bila kumsahau mchora katuni wetu Nathan Mpangala.

Ni wazi kuwa taarifa nyingi za Kamati zinazoundwa huwa ni ndefu na hivyo kuwapelekea wananchi wa kawaida ambao ni wadau muhimu sana katika jamii kushindwa kusoma au kutoielewa kabisa kutokana na lugha inayotumika. Hii ilipelekea Policy Forum kuamua kuandaa tafsiri rahisi ya taarifa hiyo kwa kutumia lugha rahisi na vielelezo kama katuni.

Sote tunafahamu Tanzania imebarikiwa neema ya madini ya aina mbalimbali yaliyopo nchini pote. Lakini pamoja na kujaliwa wingi wa madini mbalimbali bado inaonekana kuwa sekta ya madini haichangii vya kutosha katika maendeleo ya nchi hasa ya kiuchumi na kijamii na pia kuonekana kuwa mikataba ya madini inapendelea zaidi kampuni kubwa za uwekezaji katika madini, ikiwemo usiri mkubwa wa mikataba hiyo.

Ni matarajio yetu kuwa tafsiri hii rahisi ya taarifa ya kamati ya madini itawasaidia watanzania wote kuelewa kinachoendelea katika sekta ya madini na mapendekezo ya kamati kama yalivyoainishwa.

Ni matumaini yetu pia kuwa kitabu hiki kitaongeza uelewa kwa wadau wote juu ya umuhimu wa kuikuza sekta hii muhimu na vile vile kujua kinachoendelea katika sekta ya madini kwa ujumla.

Soma zaidi