Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Sheria hii mpya ya madini imetungwa baada ya mchakato mrefu uliotanguliwa na Kamati na tume mbalimbali zilizoundwa pamoja na msukumo mkubwa kutoka asasi za kiraia na kuhitimishwa na Tume iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani iliyoundwa mwaka 2007. Sheria hii inaweka utaratibu wa kisheria katika kutekeleza sera mpya ya madini ya mwaka 2009. Sheria hii ya madini namba 14 ya mwaka 2010 ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Aprili 2010 na kusainiwa na Rais tarehe 20 Mei, 2010. Ni matumaini yetu kuwa tafsiri hii rahisi (siyo ya moja kwa moja) itaongeza uelewa wa wananchi wa kawaida juu ya kilichomo kwenye sheria husika ambayo ni kubwa na imeandikwa kwa lugha ngumu ya kisheria ya kiingereza. Huu ni mwendelezo tu wa juhudi ambazo Policy Forum imekuwa ikifanya kwa kutafsiri sheria na sera mbalimbali kwa lugha rahisi ya Kiswahili. Chapisho la kwanza lilitolewa mwaka 2007 mara baada ya kutolewa kwa sheria ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (PCCA) Sheria Namba 11 ya 2007. Chapisho la Pili lilitoka
mwaka 2010 ambalo lilihusu sheria zinazohusu Rushwa katika Chaguzi ambalo tulilitoa kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2010. kusoma zaidi tafadhali angalia kiambatanisho hapo chini. Bofya hapa