Moses Kulaba, Mwakilishi wa kikundi kazi cha bajeti akiwa anatoa mada Stockholm tarehe 23 Septemba
Tarehe 23 Septemba kikundi kazi cha Bajeti(BWG) cha Policy Forum kilialikwa na Forum Syd na Svenska Institutet kutoa neno katika semina ya asubuhi iliyohusu ukwepaji haramu wa mitaji katika nchi maskini, jinsi gani inaathiri maendeleo, na jinsi gani inaweza kusimamishwa.
Mada ilitoka katikati ripoti mpya ambayo Kikundi kazi cha bajeti cha Policy Forum kilikuwa mwandishi mwenza.
Kinachoitwa "Bringing the Billions Back: How Africa and Europe can End Illicit Capital Flight" kinachoeleza ripoti ya mitaji haramu, jinsi ya kuiteketeza, ukubwa wake, matokeo yake kwa maskini, na hatua zinazohitajika ili kuitokomesha.Muwakilishi wa kikundi kazi chaa bajeti alietoa neno alikuwa Moses Kulaba.
Wasemaji wengine katika semina hiyo walikuwa Kristina Fröberg, mtaalamu wa siasa na afisa utetezi wa Forum Syd, mtandao wa mashirika karibu 200 ya kiswedish ya kiraia katika kushirikiana kwa ajili ya haki katika dunia, na Dk Attiya Waris, mhadhili katika Taasisi ya Sheria katika Chuo Kikuu ya Nairobi na pia mwanachama wa OECD na pia makamu mwenyekiti wa Mtandao wa Haki ya Kodi.