Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Kama sekta ya kilimoTanzania itawekezwa ipasavyo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Kwa mujibu wa taarifa ya bajeti 2011/12 iliyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya kilimo, kwa sasa sekta hii ina ajiri asilimia 77.5 ya watanzania na kuchangia asilimia 95 ya chakula kinachotumika nchini. Sekta ya kilimo pia inaonekana kukua kwa asilimia 4.2 tangu mwaka 2010 kutoka asilimia 3.2 ya mwaka uliotangulia. Baada ya serikali kutambua mchango mkubwa wa sekta ya kilimo kwa maisha ya watanzania wengi, kuanzia mwaka 2006/7 iliamua kutekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) kwa kiasi kikubwa kupitia Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Wilayani (DADPs). tangu kipindi cha mwaka (2006/2007 – 2011/12, bajeti halisi ya sekta ya kilimo imeongezeka kutoka shilingi 276.6 bilioni za kitanzania hadi shilingi 926 billioni. Kusoma zaidi bonya namba 1 na 2