Mitiririko Haramu ya Fedha (IFFs): Mzigo kwa Bajeti ya Taifa la Tanzania
Mitiririko haramu ya fedha (IFFs) ni changamoto kubwa kwa utengemano wa kiuchumi, hufanya nchi ipoteze mapato makubwa ambayo yangetumika katika kuendeleza sekta muhimu kiuchumi kama vile kilimo. Huu muhtasari wa kisera unachunguza athari ya mitiririko haramu ya fedha (IFFs) katika bajeti ya taifa la Tanzania, kwa kuzingatia sekta ya kilimo. Muhtasari huu unaonesha jinsi fedha zilizopotea kutokana na mitiririko haramu ya fedha zingeweza kuziba pengo la upungufu wa bajeti ya sekta ya kilimo, pia unatoa mapendekezo ya msingi ili kutatua tatizo hili. Pakua PDF kusoma zaidi.