Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Wadau wa habari, ikiwemo mtandao wa Policy Forum, wametoa tamko kuhusu azma ya serikali kupeleka miswada ya Haki ya Kupata Habari (Access to Information Bill) na Huduma za Vyombo vya Habari (Media Services Bill) kwa Utaratibu wa Hati ya Dharura.

Tamko lao linatoa wito kwa serikali kusitisha uwasilishwaji wa miswada hiyo miwili kwa utaratibu wa hati ya dharura ili kuwapa fursa wadau na wananchi kuisoma, kuichambua na kutoa maoni yao. Wadau hao pia wametoa wito kwa serikali kutumia mkutano wa 19 wa Bunge la Tanzania kusoma miswada hii kwa mara ya kwanza kama hatua ya kuitayarisha kupokea maoni ya wadau kwa miezi inayokuja.

Kwa Bunge la Tanzania, wadau wameitaka kutokubali kupokea na kujadili miswada hii kwa utaratibu wa hati ya dharura.

Kusoma tamko kamili, bofya hapa.