Skip to main content

Mkutano Wa Uwazi Katika Usimamizi Wa Fedha Wavuta Hadhira Ya Kimataifa

Imechapishwa na Policy Forum

Mtandao wa Uwazi Katika usimamizi wa Fedha “The Financial Transparency Coalition (FTC)’ na asasi mwenyeji ya Policy Forum, wameandaa mkutano mahiri katika uwazi wa usimamizi wa fedha. Mada kuu ya mkutano huo wa siku mbili unaofanyika Jumanne  na Jumatano wiki hii katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, ni “Kuleta Uwazi: Namna ya Kujenga Uwazi wa Matumizi ya Fedha Duniani kwa Ajili ya Maendeleo”.

Tamko La Kikundi Kazi Cha Bajeti Cha Policy Forum Juu Ya Taarifa Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Serikali (Cag) Ya Mwaka 2011/2012

Imechapishwa na Policy Forum

Juma lililopita, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) aliwasilisha Bungeni taarifa yake ya  mwaka kuhusu mahesabu ya serikali kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2012 kufuatana na ibara ya 143  ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 34 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na: 11 ya mwaka 2008.  Taarifa inaonyesha baadhi ya masuala ambayo yanazuia ufanisi wa Serikali kuu, Serikali za mitaa, Mamlaka za umma na vyombo vingine kufikia malengo yao.

Policy Forum Kushiriki katika semina ya asubuhi ya ukwepaji haramu wa mitaji katika nchi maskini iliyofanyika sweden

Imechapishwa na Policy Forum

Moses Kulaba, Mwakilishi wa kikundi kazi cha bajeti akiwa anatoa mada Stockholm tarehe 23 Septemba                                                       

Tarehe 23 Septemba kikundi kazi cha Bajeti(BWG) cha Policy Forum  kilialikwa na Forum Syd na Svenska Institutet kutoa neno katika semina ya asubuhi iliyohusu ukwepaji haramu wa mitaji katika nchi maskini, jinsi gani inaathiri maendeleo, na jinsi gani inaweza kusimamishwa.               

Mada ilitoka katikati ripoti mpya ambayo Kikundi kazi cha bajeti cha Policy Forum kilikuwa mwandishi mwenza.

Subscribe to Transparency