Vinara wa Uwajibikaji Wajengewa Uwezo Kuhusu Mfumo Ulioboreshwa wa O&OD na Mchakato wa Bajeti katika Ngazi ya Msingi
Vinara wa Uwajibikaji (Community Accountability Champions – CACs) kutoka wilaya za Tanganyika mkoani Katavi na Mpwapwa mkoani Dodoma wamejengewa uwezo kupitia mafunzo maalum yaliyoratibiwa chini ya mradi wa Raia Makini, unaotekelezwa na Wajibu – Institute of Public Accountability kwa kushirikiana na Policy Forum, kwa ufadhili wa pamoja kutoka Umoja wa Ulaya (EU).