Makosa ya Rushwa Katika Chaguzi Tanzania
Policy Forum na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tunakuletea tena chapisho hili la tatu katika mtiririko wa machapisho yanayohusu elimu kwa umma juu ya kupambana na rushwa.
Mtakumbuka kuwa chapisho letu la kwanza la pamoja lilihusu sheria mpya namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa hapa Tanzania,
Chapisho hili linaweka wazi sheria zetu zinavyosema kuhusu makosa yarushwa katika chaguzi hapa nchini Tanzania na adhabu zinazotolewa kwa makosa husika,