Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Kazi hii na nyingine nyingi zilizofanyika katika Mwaka 2014 zisingefanikiwa bila michango ya kiufundi, mawazo, maoni, ushauri, hali na mali kutoka kwa wadau, marafi ki na wawezeshaji mbalimbali. Ni jambo la kheri kuwa miaka minne ya maisha ya JUKWAA LA KATIBA TANZANIA imekuwa ya harakati, kazi na mafanikio makubwa kiasi hiki. Shukrani na pongezi nyingi ziwaendee wote walioamua kufanya kazi bega kwa bega na JUKATA kwa miaka yote tangu kuanzishwa rasmi kwa JUKATA na hasa katika mwaka wa 2014 hadi kukamilisha Kijitabu hiki

muhimu.

Kwanza, kulikuwa na watu waliokubali kuwa sehemu ya kikosi kazi cha uchambuzi wa Katiba Inayopendekezwa. Kikosi hiki kilihusisha Wanasheria na wachambuzi wa masuala la Katiba, Siasa na Sera ambao walijifungia na kufanya uchambuzi wa kina wa Katiba inayopendekezwa huku wakilinganisha na Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977. Kipekee, tunawashukuru sana mwanasheria Mwassa Jingi, Mwanasheria Christina Kamili, Mchambuzi Hebron Mwakagenda, pamoja na wataalam wengine kutoka Sekretarieti chini ya

uongozi wa Mratibu wa JUKATA, Diana Kidala na maofi sa wake wakiwemo: Mchereli Machumbana, Lilian Mushi na Rosency Kabyemera. Pamoja nao, mchora Katuni mashuhuri, Muhidin Msamba aliweka nakshi katika Kijitabu hiki kwa kuchora Katuni ambazo zinafanya sura ya chapisho hili kuwa ya kipekee.Kusoma zaidi bofya hapa.