Skip to main content

The Sustainable Hub for Policy Initiates (SHPI)

Imechapishwa na Policy Forum

Sisi ni Shirika lisilo la Kiserikali lililoanzishwa kwa lengo la kuendeleza maendeleo. The Sustainable Hub for Policy Initiatives (SHPI) inaamini kwamba utawala bora ni sehemu muhimu ya kupata maendeleo endelevu ambayo hutoa kupunguza umaskini.

The Sustainable Hub for Policy Initiatives (SHPI) imejitolea kufikia malengo ya maendeleo endelevu, maono ya muda mrefu ya taifa, mikakati, na sera za kitaifa, hivyo basi shirika limefafanua utawala bora kama lengo kuu.

Kazi zinazofanywa na SHPI:

Mtazamo wa Azaki Kuhusu Siku 100 za Magufuli Madarakani

Imechapishwa na Policy Forum

Kabla ya uchaguzi mkuu  wa Oktoba 25, 2015, Asasi Za Kiraia (AZAKI) chini ya Kikundi Kazi  cha Bajeti cha  Policy Forum ziliandaa na kuwasilisha kijarida kinachoitwa“Vipaumbele  Vyetu Vikuu  kwa Serikali Ijayo”  kwa  vyama mbalimbali vya siasa  vilivyokuwa vinashiriki katika uchaguzi ili kutilia mkazo yaliyomo kwenye kijitabu hicho.  Kijarida hicho kilikuwa na masuala nyeti yaliyohitaji serikali ya awamu ya tano kuzingatia.  

Tamko La Asasi Za Kiraia Kuhusu Viashiria Vya Uvunjifu Wa Amani Wiki Moja Kuelekea Tarehe Ya Upigaji Kura Katika Uchaguzi Mkuu Tanzania Tarehe 25.10.2015

Imechapishwa na Policy Forum

Asasi za Tanzania tumeendelea kufuatilia mchakato wa uchaguzi mkuu 2015 tangu uandikishaji wapiga kura, uhamasishaji hadi kampeni zinazoendelea kwa umakini mkubwa. AZAKI tumefanya hivyo tukiamini kuwa uchaguzi  ni sehemu kuu ya michakato ya kidemokrasia hapa nchini kama ilivyo duniani kote. Sisi asasi za kiraia Tanzania, tukiwa watetezi na wasimamizi wa demokrasia, utawala bora na haki za binadamu, hatumuungi mkono mgombea yeyote wala chama chochote cha kisiasa kinachotafuta kuingia madarakani wala hatulengi kuchukua dola.

Utawala wa Kidemokrasia Katika Jamii (Toleo la 8)

Imechapishwa na Policy Forum

UTANGULIZI

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi.

Miswada Ya Takwimu Pamoja Na Makosa Ya Mtandao, 2015

Imechapishwa na Policy Forum

Sisi, wanachama wa Policy Forum, Mtandao  wa mashirika yasiyo ya kiserikali, tuliokutana tarehe 29 na 30 Aprili, 2015 katika mkutano wetu wa mwaka (AGM) Dar es salaam, tumesoma na kuchambua kwa kina Miswada ya  Sheria ya Takwimu pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kwa lengo la kujieleimisha na masuala ya katiba na uchaguzi mkuu 2015.

1.       SHERIA YA TAKWIMU NA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI

Subscribe to Good Governance