Skip to main content

Utawala wa Kidemokrasia Katika Jamii (7th Edition)

Imechapishwa na Policy Forum

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi. Kusoma bofya hapa

Mwongozo wa Utawala Bora

Imechapishwa na Policy Forum

Kijitabu hiki cha Mwongozo wa Utawala Bora ni mfululizo wa utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na Policy Forum ya kukuza utawala bora nchini. Vile vile, kijitabu hiki ni mchango wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na Policy Forum katika kusaidia juhudi za Serikali za kuimarisha utawala bora katika ngazi zake zote.

Kukisoma bofya hapa

Ujumbe kutoka Tanzania kwa Obama: Uwazi hujenga taasisi yenye nguvu

Imechapishwa na Policy Forum

Rais wa Marekani Barack Obama na vyombo vya habari wanaweza kusafiri kuja katika nchi yangu wiki hii kwa majadiliano juu ya masuala  ya 'mvuto' kama  ya ushindani wa kiuchumi wa  Marekani na China au amani na masuala ya usalama. Hata hivyo kama   kweli Marekani  ipo makini kuhusu kusukuma utawala wa kidemokrasia duniani kote, ni  mambo  haya madogo ya 'mvuto'  ambayo ni muhimu zaidi.

Documentary ya Miaka Kumi ya Policy Forum ya Ushawishi na Utetezi wa Sera

Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum imeadhimisha miaka yake kumi ya ushawishi na uchechemuzi wa sera tokea ianze rasmi mwaka 2003, maadhimisho hayo yalifanyika katika mkutano wake mkuu wa mwaka pamoja na wanachama wake.

wanachama hao walionyeshwa documentary fupi inayoonyesha historia ya Policy Forum tokea ianze, changamoto ilizopitia na jinsi ambavyo ilikumbana na hizo changamoto, baada ya hapo baadhi ya wanachama wa Policy Forum  walieleza jinsi ambavyo wamefaidika kwenye mtandao huo.

Kuona documentary hiyo tafadhali bofya hapa

Tamko La Kikundi Kazi Cha Bajeti Cha Policy Forum Juu Ya Taarifa Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Serikali (Cag) Ya Mwaka 2011/2012

Imechapishwa na Policy Forum

Juma lililopita, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) aliwasilisha Bungeni taarifa yake ya  mwaka kuhusu mahesabu ya serikali kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2012 kufuatana na ibara ya 143  ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 34 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na: 11 ya mwaka 2008.  Taarifa inaonyesha baadhi ya masuala ambayo yanazuia ufanisi wa Serikali kuu, Serikali za mitaa, Mamlaka za umma na vyombo vingine kufikia malengo yao.

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii

Imechapishwa na Policy Forum

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kwa taarifa kamili tafadhali bofya hapa.

Subscribe to Good Governance