Skip to main content

Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II): Ni kwa Jinsi Gani Tutaboresha Utekelezaji Katika Mamlaka ya Serikali za Mtaa?

Imechapishwa na Policy Forum

Mwanzoni mwa mwaka 2016, Serikali ilizindua FYDP II, kwa lengo la kurekebisha mapungufu ya FYDP I na kutoa mpango makini wakati Tanzania inapoanza kuelekea katika maendeleo ya viwanda katika miaka mitano ijayo (2016 – 2021).

Katika kufanya marejeo ya FYDP I, serikali ilitambua kuwa mpango wa awali ulishindwa kufanikisha malengo yake mengi. Wakati Serikali imedhamiria kuwa ukuzaji wa viwanda ni kipaumbele katika miaka mitano ijayo, mapungufu ndani ya mpango unaweza kufanya nchi ishindwe kwa mara nyingine tena kama masuala yaliyojitokeza hayajafanyiwa kazi vya kutosha.

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini

Imechapishwa na Policy Forum

Mwongozo huu umetolewa na Policy Forum katika jitihada zake za kurekodi yale yaliyojiri waliposhirikiana na wabunge katika kuchangia sheria mpya ya madini Tanzania, na kuboresha uwezo wa asasi za kiraia na vyombo vya habari katika kusimamia utendaji wa serikali kwenye sekta ya uziduaji (mafuta, gesi asilia na madini). Programu hii ilifanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Revenue Watch. Kusoma zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini. bofya hapa

Mkakati wa Pamoja wa Uratibu na Matumizi bora ya Misaada

Imechapishwa na Policy Forum

Mchakato wa kuhalalisha mahusiano baina ya Serikali, wahisani, wafadhili na Asasi zizo za kiserikali AZAKI umekuwa na changamoto nyingi. Kumekew na juhudi nyingi ambazo zimekuwa zikitoa tumaini kwa AZAKI kwamba mahusiano rasmi na wadau wengine wa maendeleo ni jambo ambalo linawezekana kuwa rasmi na endelevu.

Ukuaji wa Uchumi Tanzania: Je, Unapunguza Umaskini?

Imechapishwa na Policy Forum

Tanzania imesifiwa sana kuwa inaendesha uchumi wake katika njia sahihi. Katika chapisho la hivi karibuni, “Tanzania: the story of an African transition”, shirika la fedha duniani IMF, linadai kuwa katika miongo miwili iliyopita, uchumi wa Tanzania umepitia kipindi cha mpito chenye mafanikio, ambapo uchumi huria na mageuzi ya kitaasisi yamepelekea kuongezeka kwa pato la taifa hadi kufikia zaidi ya 7% kwa mwaka tangu 2000. bofya hapa

Taarifa Ya Hali Ya Uchumi Wa Taifa Kwa Mwaka 2008 Na Malengo Katika Kipindi Cha Muda Wa Kati (2009/10-2011/12)

Imechapishwa na Policy Forum

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa likae kama Kamati ili liweze kupokea na kujadili Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika kipindi cha mwaka 2008 na malengo katika kipindi cha Muda wa Kati (2009/10 – 2011/12). Pamoja na hotuba hii, nawasilisha Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2008; na Kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2009/10. bofya hapa

Msimamo wa Wanachama wa Policy Forum kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo

Imechapishwa na Policy Forum

Wanachama wa Policy Forum, tukiwa ni sehemu ya jumuiya za kiraia na sehemu ya wapiga kura wa wabunge wetu tumechukua jukumu katika jukwaa hili leo kutoa tahadhari kwa wabunge wetu kuhusu athari za kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya jimbo. Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea maendeleo endelevu nchini kwetu. Bila mjadala mpana na mawazo chanya yaliyochambua maswala kwa undani kama msingi wa maamuzi, nchi itafanya maamuzi dhaifu yasiosimama kwenye misingi ya hoja na ukweli wa mambo.

Mkutano wa ufuatiliaji matumizi ya fedha za umma Afrika Mashariki

Imechapishwa na Policy Forum

Katika miaka kumi iliyopita, asasi za kiraia katika nchi zaidi ya 60 duniani zimeanzisha mikakati ya kuchunguza jinsi serikali zao zinavyotumia pesa za umma. Harakati hizi zimefikia kuangalia kila hatua katika ya mchakato wa bajeti: mipango, utengaji wa mafungu, matumizi na matokeo ya matumizi. 

Subscribe to Development