Skip to main content

Jukwaa issue 3

Imechapishwa na Policy Forum

This issue is on the topic of decentralisation. Where is Management of Public Money Most Accountable - at Central or Local level?. bofya hapa kuisoma

Community Development for All (CODEFA)

Imechapishwa na Policy Forum

Community Development for All (CODEFA) ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kuboresha usawa na ustawi wa uchumi endelevu wa jamii za Tanzania Bara. CODEFA hufanya kazi ya kuongeza uelewa katika ngazi za chini na kuwezesha jamii kuchambua kwa kina hali zao, kutambua fursa na vizuizi kwa maendeleo, na kujipanga kwa pamoja  ili kujiletea maendeleo. Lengo kuu ni kuwezesha jamii zilizo pembezoni na zilizo katika mazingira magumu kushiriki kikamilifu katika kutokomeza umaskini.

Kazi zinazofanywa na CODEFA:

Community for Sustainable Development

Imechapishwa na Policy Forum

Community for Sustainable Development huwezesha jamii kutetea haki za watoto ikiwa ni pamoja na msaada wa elimu kwa watoto yatima, watoto walio katika mazingira magumu zaidi, elimu ya afya ya mama, ulinzi wa watoto, vijana na haki za kimsingi za wanawake kupitia sheria na sera mbalimbali. Pia ni asasi inayojishughulisha na masuala ya usawa wa kijinsia, uhifadhi wa mazingira , utawala bora na uwajibikaji wa kijamii na stadi za maisha ya kijamii, 

Tushiriki

Imechapishwa na Policy Forum

Tushiriki imejitolea kushiriki katika kuleta maendeleo ya jamii masikini nchini Tanzaia. Pia ni asasi inayojishughulisha na masuala ya utawala bora, maswala ya jinsia, sera ya elimu, kilimo, PET, SAM, uharibifu wa mazingira, afya, lishe, usafi , haki za binadamu, na maji safi.

Biharamulo Originating Economic Development Association (BOSEDA)

Imechapishwa na Policy Forum

Biharamulo Originating Economic Development Association (BOSEDA) ni NGO iliyosajiliwa ambayo inashirikiana kwa karibu na wadau wengine kutoa huduma zinazokidhi mahitaji kwa jamii katika sekta za Elimu, Afya, Uhifadhi wa Mazingira, Sera za kitaifa, Jinsia, Haki za Binadamu, Utawala Bora na Demokrasia pamoja na elimu ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo za ndani.

Subscribe to Development