Skip to main content

Mapitio ya " Suala la Dola Bilioni Moja": Tanzania Inaendelea Kupoteza Kiasi Gani cha Fedha za Kodi?

Imechapishwa na Policy Forum

Serikali inalo jukumu kubwa la kuwahakikishia na kuwapatia watu wake huduma na bidhaa za umma. Hizi ni pamoja na afya, elimu, maji, miundombinu, ulinzi na usalama na kadhalika. Huduma na bidhaa hizi ni muhimu sana ili wananchi waweze kustawi na kuondokana na matatizo kama vile umaskini, ujinga na maradhi.Huduma na bidhaa za umma hugharimu rasilimali nyingi zikiwemo fedha. Fedha hizi ni za kutoka ndani na nje ya nchi. Fedha za ndani ni pamoja na mapato ya kikodi na yasiyo ya kikodi.

Maelezo ya Ripoti ya Mbeki Kuhusu Uhamishaji Haramu wa Fedha kutoka Barani Afrika

Imechapishwa na Policy Forum

Februari 2015 Jopo la Ngazi ya Juu Kuhusu Uhamishaji Haramu wa Fedha kutoka Barani Afrika, likiongozwa na Mwenyekiti wake Rais Thabo Mbeki, liliwasilisha ripoti yake kwa Tume ya Umoja wa Afrika/Tume ya Umoja wa Kimataifa ya Kiuchumi Barani Afrika (AUC/ECA). Ripoti ilionesha kuwa nchi za Kiafrika hupoteza kwa wastani dola bilioni 50 kwa mwaka kutokana na uhamishaji haramu wa fedha. Shughuli za kibiashara za sekta binafsi ndizo zinazochangia kwa kiwango kikubwa uhamishaji haramu wa fedha (IFFs), zikifuatiliwa na uhalifu uliopangwa, kisha shughuli za sekta ya umma.

Tamko La Kikundi Kazi Cha Bajeti Cha Policy Forum Juu Ya Taarifa Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Serikali (Cag) Ya Mwaka 2011/2012

Imechapishwa na Policy Forum

Juma lililopita, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) aliwasilisha Bungeni taarifa yake ya  mwaka kuhusu mahesabu ya serikali kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2012 kufuatana na ibara ya 143  ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 34 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na: 11 ya mwaka 2008.  Taarifa inaonyesha baadhi ya masuala ambayo yanazuia ufanisi wa Serikali kuu, Serikali za mitaa, Mamlaka za umma na vyombo vingine kufikia malengo yao.

Nioneshe Pesa Ziliko

Imechapishwa na Policy Forum

Katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la madai ya uwajibikaji kutoka kwa Wabunge ambayo yamebadilisha muonekano wa Bunge na yamepelekea kujiuzuru kwa mawaziri kadhaa, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu. Mswada wa Sheria ya Ukaguzi imepelekwa Bungeni chini ya hati ya dharura na itajadiliwa katika kikao kijacho cha Bajeti mwaka huu. Mswada huu unalenga kuiongezea Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAO) uhuru mkubwa wa kutoingiliwa na Dola katika utendaji wake wa kumsaidia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Subscribe to Revenues