Skip to main content
Mjue Diwani

Nchi yetu imekuwa ikifanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali wakiwemo Rais, Wabunge na Madiwani kila baada ya miaka mitano au kwa mujibu wa sheria pale itakapo hitajika. Wananchi hupata nafasi ya kuelimishwa umuhimu wa kushiriki uchaguzi kwa kupiga kura au kuwa wagombea wa nafasi mbalimbali. Haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya msingi inayotolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uongozi wa Kidemokrasia katika Jamii: Ushiriki wa Wananchi na Viongozi katika Ngazi za Msingi za Serikali za Mitaa

Ushiriki wa wananchi ni suala muhimu na la msingi sana katika kujiletea maendeleo yao katika vijiji na mitaa. Mahali ambapo wananchi hawashiriki wala hawashirikishwi kunakuwa na lawama na mizozo mingi kwa viongozi hasa pale ambapo maamuzi yaliyopitishwa yanawaumiza wananchi ndipo tunaona umuhimu wa kushiriki unajitokeza zaidi.

Tamisemi Kushirikiana na AZAKI kuandaa Mwongozo wa Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu Wenye Ulemavu

Imechapishwa na Policy Forum

Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/2017-2020/21), pamoja na malengo mengine, unakusudia kuweka mazingira wezeshi kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujiajiri na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo kama vile uvuvi, kilimo, ufugaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na Serikali ya kutimiza lengo la kusaidia makundi hayo ni utoaji wa mikopo isiyo na riba.

Zijue Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa: Ngazi ya Vijiji, Mitaa na Vitongoji, 2019

Imechapishwa na Policy Forum

 Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8(1) (a); wananchi ndio chimbuko la mamlaka ya utawala wa nchi na kwamba Serikali itapata mamlaka kutoka kwao. Uchaguzi ndio namna pekee ya wananchi kukasimisha mamlaka yao kwa viongozi. Ni Haki ya kila raia kushiriki katika michakato ya Uchaguzi ikiwemo kupiga au kupigiwa kura kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi ili kupata viongozi.

Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini: Mfumo wa Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG)

Imechapishwa na Policy Forum

Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya tathmini ya mwaka na ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa shughuli zinazogharamiwa na Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG) kama zinavyotekelezwa mara kwa mara na Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Uhusiano huu unatokana na ukweli kwamba ufuatiliaji unaopaswa kufanywa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa unagusa kwa kiwango kikubwa masuala yaleyale au maeneo muhimu ambayo hufanyiwa tathmini wakati wa upimaji wa mwaka.

Mwongozo wa Utekelezaji na Uendeshaji: Mfumo wa Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG)

Imechapishwa na Policy Forum

Serikali imedhamiria kutekeleza Sera ya Ugatuaji wa Madaraka ambapo moja ya mambo ya msingi katika Sera hiyo ni ugatuaji wa masuala ya fedha kupitia eneo hili. MSM zinawezeshwa kifedha kufanya maamuzi yanayohusu maeneo yao ili kukidhi mahitaji yaliyobainishwa kwenye maeneo yao na kutekeleza programu na shughuli zinazotokana na mahitaji hayo. Kwa hiyo, ugatuaji wa masuala ya fedha, una maana kwamba MSM zinawekewa masharti ya kifedha kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yao kupitia mapato ya ndani na mapato kutoka Serikali Kuu kwa uwazi na usawa.

Hotuba Ya Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa (Or-Tamisemi) Mhe. Selemani Jafo (Mb) Wakati Wa Uzinduzi Wa Miongozo Ya Mfumo Wa Utoaji Wa Ruzuku Ya Maendeleo Ya Serikali Za Mitaa (Lgdg) Mjini Dodoma, 28 Oktoba 2017

Imechapishwa na Policy Forum

HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OR-TAMISEMI) MHE. SELEMANI JAFO (MB) WAKATI WA UZINDUZI WA MIONGOZO YA MFUMO WA UTOAJI WA RUZUKU YA MAENDELEO YA SERIKALI ZA MITAA (LGDG) MJINI DODOMA, 28 OKTOBA 2017

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma,

Wenyeviti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na Bahi,

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma,

Kikundi Kazi Cha Policy Forum Na Or-Tamisemi Wajadiliana Jinsi Ya Kuboresha Utendaji Katika Ngazi Za Serikali Za Mitaa Nchini

Imechapishwa na Policy Forum

Halmashauri nchini zimeshauriwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ili ziweze kupata mapato ambayo yatasaidia katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika ngazi ya serikali za mitaa. Hayo yamesemwa Oktoba 27, 2017 mjini Dodoma na wawakilishi wa idara mbalimbali za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) wakati wa mkutano uliojumuisha wanachama wa Policy Forum (PF) na maafisa wa OR-TAMISEMI.

Subscribe to Local Governance