Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

 Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8(1) (a); wananchi ndio chimbuko la mamlaka ya utawala wa nchi na kwamba Serikali itapata mamlaka kutoka kwao. Uchaguzi ndio namna pekee ya wananchi kukasimisha mamlaka yao kwa viongozi. Ni Haki ya kila raia kushiriki katika michakato ya Uchaguzi ikiwemo kupiga au kupigiwa kura kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi ili kupata viongozi. Hivyo ni muhimu Serikali kuhakikisha kwamba wanachi wanapata fursa ya kushiriki katika chaguzi huu wa Serikali za Mitaa, 2019. Soma zaidi