Ushindani wa Kodi Afrika ya Mashariki:Mbio za kuelekea chini? Motisha ya Kodi na Upotevu wa Mapato Tanzania
Serikali ya Tanzania inatoa wigo mpana wa motisha wa kodi kwa wafanya biashara ili kuvutia viwango vikubwa zaidi vya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDIs) nchini.
Utoaji wa motisha ya kodi Tanzania, tunaweza kusema ni sehemu ya ushindani wa kodi miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC). Kufuatia uundaji wa EAC mwaka 1999, Kenya, Tanzania, na Uganda walianzisha umoja wa forodha (eneo ambalo halina ushuru wa forodha na lenye kiwango cha tozo ya bidhaa zinazotoka nje ya nchi kinachofanana) mwaka 2005, na Rwanda na Burundi wakajiunga mwaka 2009.