Skip to main content

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari: Maoni Ya Kikundi Kazi Cha Bajeti Cha Policy Forum Kuhusu Bajeti Ya Taifa 2018/2019

Imechapishwa na Policy Forum

Dodoma, Julai 17 2018

Tarehe 14 mwezi wa Juni 2018 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Philip Mpango aliwasilisha Bungeni Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge ili kuruhusu utekelezaji wake ifikapo Julai Mosi 2018. Hotuba hii ya Waziri ilitanguliwa na mawasilisho ya bajeti za Wizara mbalimbali pamoja na mijadala.

Uchambuzi Wa Utekelezaji Wa Mapato Na Matumizi Ya Mwaka 2016/2017 Na Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Kwa Mwaka 2017/2018

Imechapishwa na Policy Forum

Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni sekta muhimu sana kwa uchumi na maendeleo ya nchi na Watanzania
kiujumla. Sekta hizi zimeendelea kuwa chanzo kikubwa cha kipato kwa zaidi ya asilimia 65 ya
Watanzania na nguzo muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula, na zinachangia pato la taifa
kwa zaidi ya asilimia 29 na kwa mauzo ya nje zinachangia kwa zaidi ya asilimia 24.

Tamko Rasmi:-Bajeti 2015/2016

Imechapishwa na Policy Forum

Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2015/16 kwa sasa inajadiliwa Bungeni. Bajeti nzima ya Serikali itawasilishwa na Waziri wa Fedha mara baada ya uwasilishaji na mjadala wa bajeti za wizara kukamilika. Kwa kuzingatia umuhimu wa tukio hili kitaifa, wajumbe wa  Kikundi Kazi cha  Bajeti cha Policy Forum, tunapenda kutoa mchango wetu katika mchakato huu muhimu kwa kuchangia uchambuzi wetu. 

Bajeti Ya Serikali Kwa Mwaka Wa Fedha 2014/15 Toleo La Bajeti Ya Wananchi

Imechapishwa na Policy Forum

Kijitabu cha Bajeti ya Serikali toleo la mwananchi kinatolewa kuboresha upatikanaji wa taarifa za kibajeti kwa lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma. Kinaelezea bajeti ya Serikali kwa lugha rahisi, ikitoa dondoo za mambo muhimu kwenye bajeti na kuifanya kuwa rahisi kwa mtu wa kawaida kuielewa. Sera na mipango iliyomo katika bajeti ya Serikali huathiri maisha ya wananchi kwa namna tofaut itofauti, hivyo ni muhimu kwao kuitafakari kikamilifu maana yake.

Muswada wa Bajeti, 2014

Imechapishwa na Policy Forum

Muswada huu unapendekeza kutungwa kwa sheria ya bajeti kwa lengo la kuweka mfumo wa kisheria utakaosimamia mchakato wa bajeti ya serikali kuanzia uandaaji, uidhinishaji, utekelezaji, ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa.

Tamko la Kikundi Kazi cha Bajeti Kuhusiana na Bajeti ya Mwaka 2014/15

Imechapishwa na Policy Forum

Wakati Waziri wa Fedha  anapowasilisha  Bajeti ya Taifa  kwa mwaka wa Fedha 2014/15  Bungeni  kesho, sisi  Wajumbe wa  Kikundi Kazi cha Bajeti  cha  Policy Forum, tunaowakilisha zaidi ya Asasi  70 za Kiraia tuliounganisha nguvu zetu  ili kuongeza uelewa na  ushiriki wa jamii katika uandaaji wa sera, tunapenda kutoa  mchango wetu katika mchakato huu  muhimu.   

Toleo la Bajeti ya Mwananchi lilitolewa na Wizara ya Fedha ikishirikiana na Policy Forum

Imechapishwa na Policy Forum

Ni muhimu kila mwananchi kuuelewa na kushiriki katika mchakato mzima wa kutengeneza bajeti ya nchi yao kwahiyo basi ni vema hawa wananchi kupewa taarifa/habari za kutosha.

Kwasababu hii basi Policy Forum imekuwa ikitoa kijitabu kidogo kinachoonyesha bajeti ya nchi ya miaka husika.

Mheshimiwa Likwelile katika Mdahalo wa Policy Forum wa Juni 2010 aliahidi kuwa serikali itakuwa ikitoa vijitabu hivyo vinavyoelezea bajeti husika ili mwananchi wa kawaida aweze kuelewa.

Subscribe to Budget