Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Hili ni toleo lingine la  Bajeti Toleo la Wananchi ambalo linaelezea Bajeti ya Serikali kwa mwaka  wa  fedha  2015/16  kwa  lugha rahisi  inayoeleweka  kwa wananchi.
Bajeti  ya  Serikali ina maana ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka (ikiwa ni  pamoja  na  fedha za  ruzuku zinazopelekwa  kwenye  Mamlaka  ya  Serikali  za  Mitaa) ambayo  huwasilishwa  Bungeni  ili kujadiliwa  na  kuidhinishwa katika mwaka  wa  fedha husika.  Bajeti  ya  Serikali  inakusudia  kutekeleza  sera  na  mipango  ambayo  Serikali imejiwekea ili kufikia malengo mapana ya kiuchumi. Bajeti haina maana ya takwimu tu, bali inatafsiri vipaumbele vya Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi. Kusoma zaidi bofya hapa.