Sekta ya Kilimo na Mifugo Yatajwa Kama Chachu ya Kufikia Uchumi wa Viwanda
Wanachama wa mtandao wa Policy Forum wanaounda kikundi kazi cha bajeti (BWG) wameishauri serikali kuboresha sekta ya kilimo na ufugaji ili nchi iweze kufikia azimio lake la kuhakikisha inafikia uchumi wa kati wenye kuchagizwa na viwanda. Hayo yamesemwa tarehe 4 Mei 2019 Jijini Dodoma ambapo wanachama hao walikutana na wabunge wa kamati ya bajeti na mtandao wa kupambana na rushwa wa afrika tawi la Tanzania (APNAC-TANZANIA).