Skip to main content

Risala ya Kumkaribisha Mgeni rasmi Mhe . Mohamed Omary Mchengerwa (MB), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Katika Hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha MWELEKEO WA KATIBA MPYA TANZANIA: Tulikotoka, Tulipo na Tuendako.

Imechapishwa na Policy Forum

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Omary Mchengerwa (MB)

Waheshimiwa Wabunge

Ndugu Mwenyekiti wa Bodi ya PF Bw Bakari Khamis Bakari

Ndugu Wajumbe wa Bodi ya PF

Ndugu Viongozi na watendaji wa AZAKI hasa wajumbe wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum

Ndugu Mratibu wa Policy Forum, Bw Semkae Kilonzo

Ndugu waandishi wa habari,

Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana

Masuala Ya Wananchi Katika Katiba Inayopendekezwa: Uchambuzi Linganifu Kuhusu Yaliyomo Katika Katiba Inayopendekezwa, Rasimu Ya Katiba Ya Tume Ya Mabadiliko Ya Katiba Na Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Ya Mwaka 1977

Imechapishwa na Policy Forum

Kazi hii na nyingine nyingi zilizofanyika katika Mwaka 2014 zisingefanikiwa bila michango ya kiufundi, mawazo, maoni, ushauri, hali na mali kutoka kwa wadau, marafi ki na wawezeshaji mbalimbali. Ni jambo la kheri kuwa miaka minne ya maisha ya JUKWAA LA KATIBA TANZANIA imekuwa ya harakati, kazi na mafanikio makubwa kiasi hiki. Shukrani na pongezi nyingi ziwaendee wote walioamua kufanya kazi bega kwa bega na JUKATA kwa miaka yote tangu kuanzishwa rasmi kwa JUKATA na hasa katika mwaka wa 2014 hadi kukamilisha Kijitabu hiki

muhimu.

Rasimu ya Pili ya KATIBA Inasemaje? Chapisho la Lugha Nyepesi

Imechapishwa na Policy Forum

Tanzania ipo katika mchakato wa Katiba tangu mwanzoni mwa mwaka 2011. Hatua kadhaa zimeshapitiwa katika mchakato huu muhimu kwa Taifa letu kama ifuatavyo; Kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya
mwaka 2011, kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa mujibu wa sheria, Tume kuanza kazi kwa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya, Tume kutoa Rasimu ya kwanza ya Katiba na hatimaye Rasimu ya pili
ya Katiba.

Katiba Mpya na Ufanisi wa Serikali za Mitaa Tanzania

Imechapishwa na Policy Forum

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni katiba iliyotungwa mwaka 1977. Katiba hii inaielezea Tanzania kama nchi ya kidemokrasia, inayofuata misingi na haki za binadamu na siasa yake ni ya vyama vingi. Katiba ni sheria mama ya nchi inayowawezesha wananchi kujitambua kama taifa na ya kiutawala inayoelezea mgawanyo wa madaraka na majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola.

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania - Mwongozo wa Jamii za Kiraia

Imechapishwa na Policy Forum

Bajeti kwa kawaida imekuwa ikichukuliwa kuwa ni kazi ya wataalamu, wachumi na wahasibu tu. Lakini uamuzi wa Serikali wa namna gani ya kukusanya mapato huwaathiri wananchi wote. Kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi nyingine huathiri bei za vitu vinavyotumiwa katika kaya. Uamuzi wa matumizi ya serikali ndio huweka wazi iwapo viwango vya mishahara ya walimuna iwapo kutakuwa na dawa na vifaa vya kutosha katika zahanati au la.

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania - Mwongozo wa Jamii za Kiraia

Imechapishwa na Policy Forum

Bajeti kwa kawaida imekuwa ikichukuliwa kuwa ni kazi ya wataalamu, wachumi na wahasibu tu. Lakini uamuzi wa Serikali wa namna gani ya kukusanya mapato huwaathiri wananchi wote. Kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi nyingine huathiri bei za vitu vinavyotumiwa katika kaya. Uamuzi wa matumizi ya serikali ndio huweka wazi iwapo viwango vya mishahara ya walimuna iwapo kutakuwa na dawa na vifaa vya kutosha katika zahanati au la.

Subscribe to Constitution