Tanzania imepata ukuaji mkubwa wa uchumi katika muongo mmoja uliopita. Ingawa kiwango cha umaskini nchini kimepungua, idadi kamili ya watu maskini haijapungua kwa sababu ya kiwango cha juu cha ukuaji wa idadi ya watu. Hivyo, watoto bado wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo unyanyaswaji, utapiamlo, huduma duni za afya na elimu na huduma zingine za kimsingi.
Tumejitolea kufanya kazi na watoto, familia na jamii kushinda umasikini na udhalimu. Kuanzia mwanzo wetu nchini Tanzania mnamo 1981, tumekua kuwa moja ya mashirika makubwa ya kibinadamu na maendeleo nchini, tukifanya kazi katika mikoa 14 kati ya 33 katika wilaya 41.
Tunadhamiria kuchangia katika ustawi endelevu wa wasichana na wavulana milioni 15 haswa walio hatarini zaidi.
Kazi zinazofanywa na World Vision Tanzania:
Ustahimilivu
Lengo letu ni kwamba kaya za wakulima wadogo wadogo za Kitanzania zinawapatia watoto wao njia ya maisha yenye tija.
Tunashughulikia hili kwa :
a. Kuongeza usalama wa chakula cha kaya na mapato kupitia shughuli za shambani na nje ya shamba
b. Kuboresha usimamizi endelevu wa maliasili
c. Kuboresha uwezo wa jamii kukabiliana na majanga, dharura na udhaifu
d. Kukuza mabadiliko ya fikra kupitia mtazamo wa Ulimwenguni uliowezeshwa