Semkae Kilonzo alianza kazi Policy Forum mwaka 2007 kama mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uchechemuzi anayehusika na vyombo vya habari, ikiwa ni shauku ya mtandao kuona taarifa zinazohusiana na uchambuzi wa sera zikisambazwa kwa watunga sera, asasi za kiraia na umma kwa jumla. Akiwa kama mratibu na baadaye kama Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao amekuwa akiongoza Sekretarieti katika majukumu ya kila siku ya kiofisi. Semkae pia ni mjumbe wa Kamati ya Uwazi wa Bajeti, Uwajibikaji na Ushirikishwaji Global Movement for Budget Transparency, Accountability and Participation (BTAP).
Semkae ana digrii ya Uzamili ya Uandishi wa Habari kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff, Uingereza na pia amepata mafunzo kuhusu vyombo vya Habari, Dublin Ireland na pia katika Shule ya Uandishi wa Habari Tanzania (TSJ). Semkae ni mhitumu wa mafunzo ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini. Semkae anapenda sana kuhamasisha ushiriki wa umma katika utengenezaji wa sera na matumizi ya rasilimali za umma yanayozingatia usawa.