Skip to main content

Tamko La Policy Forum Na Wadau Wengine Juu Ya; Mapendekezo Ya Kuboresha Sheria Ya Takwimu

Imechapishwa na Policy Forum

Kufuatia kupitishwa kwa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2018,  Sisi wadau kutoka Asasi za Kiraia na watafutaji, watumiaji na wasambazaji wa taarifa za takwimu tumekutana kufanya uchambuzi wa kina wa sheria hii;

Pamoja na kutambua umuhimu wa sheria hii ambayo imelenga kuzuia usambazaji/ uchapishaji wa taarifa za kitakwimu zinazoweza kupotosha umma;

Policy Forum Yafanya Mkutano na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)

Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum mnamo tarehe 10/04/2013 ilikutana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Ofisi za THBUB. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama wa Policy Forum, Sekretariati ya Policy Forum na wafanyakazi wa THBUB.

Katika hotuba ya ufunguzi Mheshimiwa Bernadeta pamoja na mambo mengine alizungumzia dhumuni na malengo ya mkutano huo ukiwa ni pamoja na kuainisha namna ya ushirikiano baina ya Tume na Policy Forum pamoja na maeneo ya ushirikiano huu. Baada ya hotuba hiyo fupi alifungua Mkutano rasmi saa 09.00 asubuhi.

Kilimanjaro Women Information Exchange and Consultancy Organization (KWIECO)

Imechapishwa na Policy Forum

Kilimanjaro Women Information Exchange and Consultancy Organization (KWIECO) linafanya kazi ya kuboresha Haki za Binadamu na masuala ya kijinsia katika maeneo ambayo inafanya kazi. Kupitia mipango yake, inakusudia kufikia watu wengi waliopembezoni na wanaohitaji huduma zake.

Legal and Human Rights Center

Imechapishwa na Policy Forum

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ni kituo cha kutetea haki za binadamu nchini Tanzania. LHRC ilianzishwa mnamo 1995 kama shirika lisilo la kiserikali, la hiari, lisilo la vyama na lisilo la faida, kwa madhumuni ya kufanya kazi kwenye masuala ya haki za kisheria na za binadamu. Kabla ya usajili wake, mnamo Septemba 1995, LHRC ilikuwa mradi wa haki za binadamu wa Mfuko wa Elimu ya Sheria Tanzania (TANLET). Kusudi lake kuu ni kujitahidi kuwezesha umma, kukuza, kuimarisha na kulinda haki za binadamu n

Subscribe to Human Rights