Tamko La Asasi Za Kiraia Juu Ya Mafanikio Na Madhara Kwa Tanzania Kuendelea Kutumia Ushauri Wa IMF
Sisi wajumbe wa Asasi za kiraia za ki-Tanzania tuliokutana leo ukumbi wa Dar es Salaam International Conference Centre, tarehe 10 Machi 2009 kwa uratibu wa mtandao wa Policy Forum, Human Development Trust na Tanzania AIDs Forum, baada ya kujadili na kutafakari kwa kina taarifa za ''mafanikio'' ya utekelezaji mipango ya IMF na sera za Tanzania ki-uchumi kwa miaka ya 2000 hadi 2008 tumebaini yafuatayo:-
1. Ni kweli takwimu zinaonesha kukua kwa uchumi kwa wastani wa zaidi ya asilimia 7% kwa kipindi tajwa,