Skip to main content

Youth Partnership Countrywide (YPC)

Imechapishwa na Policy Forum

Tangu kuanzishwa kwa YPC kwa miaka mingi imefanya kazi kupanua nafasi ya kidemokrasia ya ushiriki wa vijana na ushawishi kupitia elimu ya wapiga kura, mijadala ya umma na kuhamasisha vijana kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi za mitaa na kitaifa. YPC hutumia njia mbalimbali kufikia wadau wake, baadhi ya njia hizo majadiliano na mafunzo.

Kazi zinazofanywa na YPC:

a. Ushiriki wa vijana katika masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi

b. Kujenga jamii huru na ya kidemokrasia

Community of Volunteers for the World (CVM) – Comunità Volontari per il Mondo) AIDS Partnership with Africa (APA)

Imechapishwa na Policy Forum

CVM / APA ni shirika lisilo la kiserikali la Kiitaliano lenye zaidi ya uzoefu wa miaka 30 katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo barani Afrika na Asia. Kazi zetu zimejikita zaidi kwenye sekta za maji na usafi wa mazingira, VVU / UKIMWI, Kukuza ushirikiano wa wazawa, usawa wa kijinsia na mikopo midogo midogo.

Community Development for All (CODEFA)

Imechapishwa na Policy Forum

Community Development for All (CODEFA) ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kuboresha usawa na ustawi wa uchumi endelevu wa jamii za Tanzania Bara. CODEFA hufanya kazi ya kuongeza uelewa katika ngazi za chini na kuwezesha jamii kuchambua kwa kina hali zao, kutambua fursa na vizuizi kwa maendeleo, na kujipanga kwa pamoja  ili kujiletea maendeleo. Lengo kuu ni kuwezesha jamii zilizo pembezoni na zilizo katika mazingira magumu kushiriki kikamilifu katika kutokomeza umaskini.

Kazi zinazofanywa na CODEFA:

Subscribe to Pwani